Karibu tuendelee kupeana dondoo muhimu sana za wewe kufanikiwa kupitia biashara unayofanya. katika dondoo hizi tunaangalia makosa yanayofanywa na wafanyabiashara wengi na yanayowazuia kupata mafanikio. Pia tunaangalia changamoto zinazowazuia wafanyabiashara wengi kushindwa kufanikiwa kupitia biashara zao.

Jinsi unavyotoa huduma au bidhaa zako kwa wateja, jinsi unavyozungumza nao, jinsi unavyowapokea, kunaeleza kila kitu kuhusu biashara yako. Kwa huduma anayopata, hata kama hataambiwa chochote mteja anaweza kupata moja kati ya haya mawili;

1. Anaweza kujisikia anakaribishwa na yeye ni muhimu sana.

2. Anaweza kujisikia hakaribishwi na ni kama anafukuzwa au anaulizwa amefuata nini.

SOMA; Unapokuwa Tayari Kuingia Kwenye Ujasiriamali Fanya Vitu Hivi Vitano.

Unapotoa huduma nzuri kwa mteja, unapomjali mteja mteja anakuona wewe ni rafiki yake na anaona anakaribishwa tena na tena na atakuwa tayari kuwaambia na wengine.

Unapotoa huduma mbovu kwa mteja, mteja anaona hajaliwi, anaona anafukuzwa na wakati mwingine anaona kama anaambiwa umefuata nini hapa, hujaona sehemu nyingine?

SOMA; Wajasiriamali Wenye Mafanikio Hufanya Mambo Haya Matano Kila Siku.

Chukua mfano umekwenda kwenye mgahawa kupata chakula, una njaa sana. Umefika pale na kukaa, unaona wahudumu wanapita pita lakini hakuna anayekuuliza unahitaji huduma gani. Unakaa na kwa sababu njaa inakusumbua unamwita mhudumu na kumwambia unataka chakula. Anakusikiliza na kwenda kukuchukulia chakula, dakika tano unasubiri chakula hakiji, dakika kumi unamuona yule mhudumu anapita tena unamuuliza chakula vipi? Anakuuliza hivi uliagiza chakula gani vile?

Hebu niambie katika hali kama hiyo utajisikiaje kama mteja? Haya ni mambo yanayotokea kila siku na unayoyafanya kwa wateja wako wakati mwingine bila ya kujua.

SOMA; Hii Ni Kazi Yenye Malipo Makubwa Sana Ambayo Unaweza Kujifunza Kuifanya

Nakutakia mafanikio kwenye biashara yako.

Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.