Hiki Ndicho Kitu Pekee Chenye Nguvu Kubwa Ya Kubadilisha Maisha Yako Kabisa.

Mara nyingi katika maisha yako huwa vipo vitu vingi ambavyo ukivielewa na kuvifanyia kazi vizuri huwa vinauwezo mkubwa wa kubadilisha maisha yako na kukuletea mafanikio makubwa unayoyataka. Pamoja na kuwa vipo vitu vingi ambavyo vinauwezo mkubwa wa kubadilisha maisha yako, lakini leo katika makala hii nataka kukushirikisha kitu kimoja tu pekee ambacho kina nguvu ya kubadilisha yako  na kuwa ya tofauti kabisa.
 

Ninaposema kitu pekee nikiwa na maana kuwa hiki ndicho kitu ambacho kwa sehemu kubwa kinauwezo wa kukufanya ukawa mtu wa mafanikio siku zote au wa kushindwa. Hiki ndicho kitu kinachokufanya uwe na pesa au ukose pesa. Hiki ndicho kitu ambacho kinakufanya uwe tajiri au maskini kabisa wa kutupwa. Pia hiki ndicho kitu ambacho kinaleta utofauti wa mkubwa wa maisha hapa duniani.
Kutokana na wengi kutokukielewa ama kukitambua kitu hiki kimepelekea wao kuishi maisha magumu na ya mateso siku zote. Kwa kukijua kitu hiki itakusaidia sana wewe kuweza kupiga hatua mbele zaidi itakayokuletea mabadiliko makubwa. Hiki ni kitu ambacho kwa vyovyote vile unatakiwa kikielewa vizuri, ili kiweze kukuletea mabadiliko unayoyataka. Kitu hiki ambacho nataka ujue hapa si kingine bali ni Uchaguzi unaoufanya kila siku juu ya maisha yako.
Ili uweze kunielewa vizuri, hebu kumbuka kitu hiki. Watu wote duniani haijalishi rangi, dini, kabila au taifa wote tulikuja hapa duniani tukiwa tupu, nikiwa na maana tukiwa hatuna kitu, tulikuja kama tulivyo sisi. Ni kitu gani ambacho kilikuja kubadili maisha na kuyaona kama yalivyo sasa hivi wengine wakiwa maskini na wengine wakiwa matajiri, ni uchaguzi tuoufanya juu ya maisha yetu kila siku.
 
Kama ni kitu hiki tu rahisi ndicho kinachoweza kuleta mabadiliko katika maisha yako, kwa nini usichague kuishi maisha unayotaka kuishi, badala ya kukaa tu na kuamuliwa na mazingira ambayo yanaweza kukupeleka kokote kule? Kwanini uendelee kulaumu kila siku maisha ni magumu sina, pesa, sina kile wala kile na kuumia tu bure? Kaa chini na ufanye uamuzi wa maana juu ya maisha yako leo unataka yaweje. 
Ukweli ni kwamba wewe ndiye unayeamua maisha yako unataka yaweje.  Wewe ndiye unayechagua na sio mtu mwingine. Tabia ulizonazo ni uchaguzi wako, kufikiri kwa namna fulani, kutafsiri kwa namna fulani matukio yanayokukuta maishani mwako, vyote ni uchaguzi wako. Unaweza ukasingizia mazingira na hali mbalimbali, kwamba ndivyo vimekufanya uwe hivyo kama ulivyo, lakini ukweli unabaki palepale, wewe ndiye unayechagua maisha yako yawe vipi. 
Kwa sehemu kubwa, mambo unayoyafanya na yanayopelekea maisha yako kuwa magumu unayafanya siku zote kwa mazoea sana. Umezoea kufikiri kwa namna fulani, kutenda kwa namna fulani, kiasi kwamba umefikia mahali unaamini kwamba, aina ya maisha uliyomo ndiyo ndiyo unayotakiwa uwe nayo. Kwa kuamini hivyo, ndivyo hivyo unakuwa umeshachagua maisha unayotakiwa kuishi haijalishi yawe ya mafanikio au ya kushindwa.
Kumbuka siku zote kuwa kufanikiwa au kutokufanikiwa maishani ni suala la uamuzi wako mwenyewe, kama vile unavyoamua kuoga au kutooga asubuhi kabla hujatoka nyumbani kuelekea kazini kwako na mafanikio yapo hivyohivyo. Ninaposema ni suala la uamuzi si maanishi uamue leo kufanikiwa na kesho uwe tajiri, hapana. Mafanikio yanakutaka wewe uanze kuweka mipango na malengo kwanza na kisha kuitekeleza.
Kama unaona unajitahidi sana maishani bila mafanikio, ni lazima urudi nyuma na kuanza kukagua tabia zako ambazo zinatokana na namna ulivyoamua kuyatazama maisha. Kama mafanikio unayoyataka hayapatikani, inawezekana ni kwa sababu umechagua aina ya maisha ambayo haiwezi kukupa mafanikio, hivyo inakubidi kukubali na kubadilika na kuingia kwenye kuchagua aina ya maisha itakayokunufaisha na kukufanikisha.
Kumbuka, kama una tabia fulani ambazo huenda ndizo zenye kukupa matokeo fulani, huwezi kuyakwepa matokeo hayo hadi uzibaini na kuziacha tabia hizo. Tabia zako zinapokuwa nyoofu, yaani ambazo hazikuumizi au kuwaumiza wengine, matokeo yake huwa pia ni mazuri. Zinapokuwa kinyume na hapo, matokeo yake huwa ni maumivu makali sana.
Kujua kile ambacho kinatakiwa kuwepo kwenye mawazo yako kila wakati ni njia ya awali ya kukuwezesha kufikia mafanikio. Kwa sababu, kama nilivyosema, wewe ndiye unayechagua uwe katika hali gani, unachagua ufanye nini na wakati gani, na huwa unafanya uamuzi huu kupitia kwenye mawazo au fikra zako. Ni muhimu kujua unafikiri kila sekende ili kuzuia kufikiri kusiko na manufaa kwako.
Kama utakuwa unaamka asubuhi na kuchagua kwamba siku itakuwa ngumu na mambo hayataenda vizuri, ni wazi huo ndiyo uchaguzi wako na ni kweli siku itakuwa ya hovyo  kwako, kumbuka unapata kwenye maisha kile ulichokichagua. Ukiamka na kufikiria kinyume na hayo ni wazi mambo yako yatakuwa mazuri. Hicho ndicho kitu pekee chenye nguvu ya kubadilisha maisha yako.
Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuboresha maisha yako.
Nakutakia mafanikio mema, endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kwa kujifunza na kuhamasika zaidi.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI NGWANGWALU,
0713 048 035,


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: