Unajua lengo la biashara ni nini?
Lengo la biashara sio kupata faida, lengo la biashara sio kupata mafanikio makubwa, haya yote ni matokeo ya lengo kuu la biashara. Yaani ukiweza kutimiza lengo hili kuu la biashara, haya mengine yote yanatimia bila ya tatizo lolote.
Biashara nyingi zinashindwa kuendelea, kupata faida na kukua kwa sababu wafanyabiashara hawajui lengo kuu la biashara. Hivyo hujikuta wakifanya biashara kwa mazoea na hivyo kushindwa kukua.
SOMA; Jinsi ya kuzuia hatari ya kupata hasara kupitia uwekezaji katika hisa
Unapojua lengo muhimu unalofanyia kazi inakuwa rahisi kwako kuangalia je kile unachofanya kitatimiza lengo au kitakutoa mbali na lengo? Kwa kujua lengo utakuwa makini na maamuzi unayofanya kila siku kwenye biashara yako.
Lengo la biashara ni kutengeneza wateja. Ndio, ukishatengeneza wateja, utapata faida, biashara itakuwa na utapata mafanikio. Lakini ukishindwa kutengeneza wateja, biashara yako inaelekea kufa, maana hakuna biashara kama hakuna wateja.
Katika lengo lako hili la biashara ambalo ni kutengeneza wateja, unahitaji kuwa na wateja wanaokuamini na watakaoendelea kufanya biashara na wewe. Na pia wateja hawa wawe tayari kuwamabia watu wengine kuhusiana na biashara unayofanya na hivyo kukuletea wateja wengi zaidi.
SOMA; MIAKA MIWILI YA AMKA MTANZANIA; Kwa Nini Ipo Na Itaendelea Kuwepo Na Mambo Mazuri Yanayokuja.
Juhudi zozote unazofanya, maamuzi yoyote unayofanya, hakikisha yanalenga kukuletea wateja zaidi wkenye biashara yako. Vinginevyo biashara itadumaa na hata kufa kabisa.
Fanyia kazi lengo lako la biashara kila siku kwa kuongeza wateja wapya kila siku.
Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.
Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.