Matumla Kumpiga Mchina Na Somo Kubwa La Kujifunza Kuhusu Mafanikio.

Siku kadhaa zilizopita kulikuwa na pambano la ngumi kati ya bondia wa Tanzania, Mohamed Matumla na bondia wa China, Wang Xin Hua. Katika pambano hili bondia wa Tanzania alimshinda kwa point bondia huyu kutoka china na hivyo kuibuka mshindi. Lengo la kuanza na habari hii sio kuonesha ubora wa bondia wa Tanzania, bali kuna somo kubwa sana la kujifunza kuhusu kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha kutoka kwenye pambano hili.

matumla

Mimi sio mtaalamu sana wa mambo haya ya masumbwi ila najua vitu viwili kwa hakika.

Kitu cha kwanza, mchezo huu wa ngumi huchezwa na mabondia wawili wenye uwezo mkubwa. Hawa ni mabondia ambao wanakuwa wamefanya mazoezi na wanakuwa kwenye kiwango sawa cha utaalamu. Yaani bondoa mwenye mkanda wa dunia hawezi kupigana na bondia ambaye anachipukia. Huyu anayechipukia inabidi apigane na wenzake wanaochipukia kwanza, awashinde, kisha apande kidogo kidogo mpaka aje amfikie huyu mwenye mkanda wa dunia ndio wataweza kupigana.

SOMA; BIASHARA LEO; Lengo La Biashara Sio Kupata Faida, Bali Ni Hili Hapa.

Kitu cha pili ni kwamba mshindi ni yule anayeweza kuvumilia kwa muda mrefu. Kama umewahi kuangalia mchezo huu sio kwmaba mshindi hapigwi na yule anayeshindwa, anapigwa sana, lakini kinachomfanya atangazwe mshindi ni uwezo wake wa kuvumilia ngumi anazopigwa na kuendelea. Kwa kuwa hawa ni mabondia ambao wana uwezo unaofanana au unaokaribiana sana, pambano haliwezi kuwa rahisi. Kila mtu atampiga sana mwenzake ila atakayetangazwa mshindi ni yule atakayedumu kwa muda mrefu, yule atakayeweza kuvumilia kwa muda mrefu.

Kama bondia mmoja atashindwa kuvumilia mapema kabla ya muda uliowekwa kumalizika basi ushindi utatangazwa haraka. Kama wote wataweza kuvumilia mpaka mwisho mshindi atapatikana kwa pointi, kulingana na uvumilivu wake katika kila hatua ya mchezo.

SOMA; Mambo Matano Ya Muhimu Kuyafahamu Kabla Ya Kuwekeza Kwenye Kilimo – 2

Je unajifunza nini katika safari yako ya mafanikio kutoka kwenye mchezo huu wa ngumi?

Kitu kikubwa kabisa ninachotaka ujufunze katika mchezo huu ni kwamba watakaopata mafanikio kwenye maisha ni wale ambao wataweza kuvumilia kwa muda mrefu. Ni hivyo tu, hakuna kikubwa zaidi ya hapo.

Jambo lolote ambalo utakwenda kufanya kwenye maisha yako, ni lazima utakutana na changamoto. Utakutana na matatizo makubwa ambayo yatakurudisha nyuma. Utakutana na watu wengi ambao watakukatisha tamaa na utakutana na kila kitu ambacho kitakwenda kinyume na vile ulivyotarajia.

Kitakachokuwezesha kufikia mafaniko sio malalamiko utakayotoa bali uvumilivu wako na kuendelea kukomaa na kufanya kile ambacho unajua ni muhimu kwako kufanya ili kufikia kile unachokitaka. Kama ilivyo kwa bondia hata kama atapigwa ngumi kiasi gani kutoka kwa mpinzani wake, lazima atakazana na yeye arudishe mapigo, tena kwa nguvu kubwa ili kuhakikisha mpinzani anapata wakati mgumu sana na kushindwa kuvumilia.

Kama kweli unataka kufikia mafanikio makubw akwenye maisha yako usiyaonee huruma matatizo na changamoto unazokutana nazo. Usiwaonee huruma watu ambao wanakurudisha nyuma. Unahitaji kupambana na unahitaji kuwa mvumilivu ndio uweze kufikia mafanikio makubwa.

SOMA; UKURASA WA 92; Usipoteze Muda Kwa Vitu Vidogo Vidogo.

Sio kitu rahisi ila pia sio kwamba haiwezekani. Matumla aliweza kumpiga mchina, ila mimi nikipelekwa kwa mchina sasa hivi siwezi kumpiga hata ngumi moja. Ila kama nikijipa muda wa kufanya mazoezi, nikaanza na mapambano madogo madogo na kuyashinda, siku moja nikipewa huyo mchina nitamgaragaza vibaya. Na hivi pia ndivyo ilivyo kwenye safari ya mafanikio. Unahitaji kuwa na maandalizi ya kutosha ili uweze kufikia kile ambacho unakitaka, maandalizi mazuri ndio yatakayokuwezesha kuwa mvumilivu.

Hakuna tatizo lolote ambalo lipo juu ya uwezo wako, sema kuna matatizo ambayo hukuwa na maandalizi mazuri ili kuweza kukabiliana nayo. Unahitaji kujijengea maandalizi mazuri ili kuwez akuvuka haya yote ambayo utakutana nayo kwenye safari yako ya mafanikio. Na kwa kuwa una uhakika kwamba lazima utakutana na matatizo, kwa nini usiwe na maandalizi ya kutosha? Hakikisha kila mara unajiandaa kwa changamoto yoyote ambayo itakuja mbele yako.

SOMA; MIAKA MIWILI YA AMKA MTANZANIA; Kwa Nini Ipo Na Itaendelea Kuwepo Na Mambo Mazuri Yanayokuja.

Hakuna watu wachache ambao walizaliwa wapate mafanikio na wengi ambao wamezaliwa ili kuwasindikiza wenye mafanikio. Kila mmoja wetu ana uwezo wake binafsi wa kufikia mafanikio makubwa. Ndio, namaanisha wewe una uwezo mkubwa sana ndani yako wa kufikia mafanikio makubwa. Kikubwa ni kuchagua na kuamua ni nini unataka, kuwa tayari kufanya kazi kwa juhudi na maarifa, kufanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya changamoto utakazokutana nazo na kuwa mvumilivu kwa lolote litakalotokea. Na maandalizi unayofanya, hufanyi kwa kusubiri uwe kamili ndio uanze, bali unaanza huku ukiendele akujiimarisha na matatizo madogo madogo utakayokutana nayo yataendelea kukuimarisha zaidi. Kama ambavyo bondia anaimarishwa na mapambano madogo madogo.

Tumia uwezo wako mkubwa na wa kipekee kuzishinda changamoto zote zitakazosimama kwenye njia yako ya kufikia mafanikio. Maandalizi, Uvumilivu.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kufikia mafanikio makubwa.

TUPO PAMOJA.

Makirita Amani

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

N;B Jipatie kitabu JINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA ambacho kitakusaidia kutumia mabadiliko kufikia mafanikio makubwa zaidi. Bonyeza jina hilo la kitabu kukipata.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: