Tunaishi kwenye dunia ambayo watu hawanunui kwa sababu tu unauza. Zamani biashara ilikuwa rahisi, uza na watakuja kununua. Fungua biashara na watu watakuja. Tangaza biashara yako kwenye vyombo vinavyowafikia wafikia wengi na utapata wateja wengi.
Ila sasa hivi mambo mengi yamebadilika. Watu hawanunui tena kwa sababu wewe unauza, hii ni kwa sababu kila mtu anauza. Watu hawanunui tena kwa sababu umetangaza sana, kila mtu anaweza kutangaza.
Mabadiliko ni makubwa sana yanayoendelea kwenye biashara. Kujua mabadiliko mengine mengi na jinsi ya kukabiliana nayo soma kitabu; Jinsi Ya kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea.
Sababu zote ambazo watu walikuwa wanazitumia kununua zamani sasa hivi zinakufa na inaibuka sababu moja kubwa sana. Sababu hiyo ni hadithi. Ni hadithi gani ambayo biashara yako inapeleka kwa wateja wake. Ni jinsi gani wateja wako watajisikia kwa kufanya biashara na wewe. Na pia wateja wako watachukuliwaje na wenzao baada ya kufanya biashara na wewe.
Wateja wanahitaji hadithi nzuri ya biashara yako. Wanahitaji kuonekana ni muhimu kwa kununua bidhaa au huduma unayotoa. Na wanapenda kuona wengine ambao wamefanya biashara na wewe wanatoa hadithi gani.
SOMA; Mambo Matano Ya Muhimu Kuyafahamu Kabla Ya Kuwekeza Kwenye Kilimo – 2
Tengeneza hadithi nzuri ya biashara yako ambayo mteja atapenda kuwa sehemu ya hadithi hiyo. Na ili uweze kutengeneza hadithi nzuri unahitaji kuchagua kundi la wateja wako, maana hadithi moja haiwezi kuwafaa watu wote.
Kama wateja wako ni vijana, hakikisha kila kijana anafurahia kuwa sehemu ya biashara yako.
Kama wateja wako ni wafanyakazi, hakikisha kila mfanyakazi anaona hii ndio sehemu pekee kwake.
Na kama wateja wako ni wazazi hakisha mzazi anayekuja anaona hapo panamfaa na atakuwa tayari kushawishi wazazi wengine nao waje hapo.
SOMA; Kama Unataka Kumaliza Matatizo Yako Ya Fedha Fanya Kitu Hiki Kimoja.
Facebook ni biashra, instagram ni biashara lakini makundi fulani ya watu yanafurahia kuwa sehemu ya biashara hii. Na wewe ifanye biashara yako iwavutie watu kuwa sehemu yake kwa sababu ya hadithi nzuri watu wanayoweza kuondoka nayo.
Hujui jinsi gani unaweza kutengeneza hadithi nzuri ya biashara yako? Tuwasiliane kwa mawasiliano yanayopatikana hapo chini.
Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.
Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.