Ni kigezo gani ambacho unatumia kupanga bei ya bidhaa au huduma zako?

Je unaangalia watu wanaweza kumudu?

Je unaangalia ni bei ipi itakuletea wateja wengi?

Je unaangalia wengine wameweka bei gani?

Vigezo vyote hivyo unawez akuvitumia ila kuna kigezo kimoja muhimu sana ambacho wengi, hasa wafanyabiashara wadogo hawakitumii. Kigezo hiki kitakuwezesha kuweka bei ambayo itakuwa nzuri kwako na kwa wateja wako pia.

SOMA; Siri Kubwa Unayotakiwa Kujua Kwenye Mahusiano Ya Kibiashara.

Kigezo hiki ni thamani unayotoa kupitia bidhaa au huduma yako.

Tumia kigezo cha thamani katika kuweka bei ya bidhaa au huduma zako. Angalia ni thamani kiasi gani ambayo mteja ataipata kw akutumia bidhaa au huduma yako na iweke hiyo kama bei.

Kama tayari umeshachagua wateja wako, yaani unalijua soko lako vizuri hakuna bei utakayoweka na watu wakaishindwa. Kikubwa ni kujua watu wanaohitaji bidhaa au huduma zako, kuwatengenezea thamani watakayokuwa tayari kuilipia na kisha kuwapatia.

SOMA; Maswali Matatu Muhimu Ya Kujiuliza Kwenye Wazo Lako La Biashara.

Soda ya kampuni moja, kwenye duka la kawaida inauzwa tsh 600/= lakini kwenye hoteli kubwa soda hiyo hiyo inauzwa tsh 3000/= na watu wananunua, bila ya kulalamika au kuomba wapunguziwe bei. Unajua ni kwa nini?

Ni kwa sababu mteja anayenunua soda kwenye hoteli kubwa anapata thamani kubwa kuliko anayenunua wkenye duka la kawaida. Watu wapo tayari kulipia thamani, kama kweli itawaridhisha.

Kazana kutengeneza thamani inayoendana na soko lako, halafu ipeleke sokoni.

Hadithi ya biashara yako pia inaweza kuongeza sana thamani ya biashara hiyo. Tengeneza hadithi nzuri ya biashara yako na watu watapend akuwa sehemu ya hadithi hiyo. Kujua jinsi ya kutengeneza hadithi nzuri soma; BIASHARA LEO; Umuhimu Wa Hadithi Ya Biashara Yako.

Wajue wateja wako, watengenezee thamani, wapatie thamani.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.