Mafanikio yako kwenye biashara yanategemea kwa kiasi kikubwa ni jinsi gani unamjua mteja wako vizuri. Kumbuka tulishakubaliana kwamba lengo lako kubwa kwenye biashara ni kutengeneza wateja na ukishaliweza hilo faida inafuata bila hata ya kuumiza sana kichwa. Nasisitiza sana hili la wateja kwa sababu ndipo udhaifu mkubwa ulipo kwa wafanyabiashara wengi wa kitanzania.

SOMA; Lengo La Biashara Sio Kupata Faida, Bali Ni Hili Hapa.

Sasa kuna mambo mengi unayotakiw akujua kuhusu mteja wako, kuanzia sifa zake, umri wake, kipato chake, mahitaji yake na mengine mengi yanayohusiana na mteja na yatakayokuwa muhimu kw abiashara yake. Naposema ujue umri wake sio lazima ujue ana miaka mingapi, ila jua yuko kwenye kundi lipi, mtoto, kijana, mtu mzima au mzee. Na pia naposema ujue kipato chake simaanishi ujue analipwa kiasi gani, ila jua kiwango cha kipato chake, kama ni cha chini, cha kati au cha juu.

Haya yote yatakuwezesha kujua utaiwekaje biashara yako ili kuweza kuenda vizuri na mteja wako.

Kitu muhimu sana unachopaswa kujua kuhusu mteja wako ni MATAGEMEO yake. Mteja kabla hajafanya biashara na wewe kuna kitu ambacho anategemea kupata kwa kile anacholipa. Ni muhimu sana kujua mategemeo ya mteja ni nini ili uweze kuyafikia. Na kama unataka mafanikio makubwa, uweze kuvuka mategemeo hayo.

SOMA; Huu Ni Uwekezaji Wa Uhakika Ambao Hautakuangusha.

Unaweza kuyajua mategemeo ya mteja kwa kuona anavyopokea bidhaa au huduma unayompatia. Kama hujayafikia ataonesha na kama umeyafikia au kuyapitiliza ataonesha pia.

Njia nyingine unaweza kumtengenezea mteja mategemeo. Hapa unamwambia mteja ni kitu gani hasa atakachopata pale atakapolipia bidhaa au huduma. Unapomtengenezea mteja wako mategemeo hakikisha sana unayafikia na hata kuyavuka. Ukifanya chini ya hapo, mteja hana sababu ya kuendelea kufanya tena biashara na wewe.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.