Kama unataka kukuza biashara yako na ifikie viwango vya juu sana basi usitegemee sana maoni ya wateja, hasa kuhusu ni nini wanataka.

Ukiondoa biashara za uchuuzi ambazo mtu anakwenda dukani moja kwa moja kununua sukari, biashara nyingi mteja hajui anachotaka. Ndio hajui ni kitu gani hasa anachokitaka, ila akikipata atafurahia sana.

SOMA; Uwekezaji Muhimu Kwako Kufanya Na Unaolipa Sana.

Sasa hili ndio lengo lako kubwa kama mjasiriamali au mfanya biashara, kujua ni nini mteja anataka, ambacho hata yeye mwenyewe hajui, na kumpatia halafu akaridhika sana.

Mteja hajui ni kitu gani anachotaka ila mteja ana matatizo. Na kama akipata kitu cha kumuondolea matatizo yake, atafurahi sana na atakuwa tayari kulipa ili aondokane na tatizo.

Wakati tulipokuwa tunatumia kanda za muziki hakuna mtu aliwahi kusema kwamba anahitaji cd, ila cd zilivyokuja na zikawa bora kuliko kanda za kawaida kila mtu alizifurahia.

SOMA; Barua Ya Wazi Kwa Vijana Wanaotafuta Ajira. Soma Hapa Uone Fursa Unazoweza Kutumia.

Kabla haijaja facebook, au twitter, au whatsapp au instagram, hatukuwahi kusikia watu wakilalamika kwamba kwa nini hakuna facebook au instagram. Lakini watu walikuwa na kiu ya kuwasiliana na wenzao walioko sehemu mbalimbali kwa haraka na kwa bei nafuu. Watu walikuwa na tatizo la kuweza kutumia nyimbo, picha na vitu vingine. Zilipokuja huduma hizi za kurahisisha mawasiliano, kila mtu amekuwa tayari kuwa mteja.

Sasa umejifunza nini katika haya yote?

Jua watu wana matatizo gani, njoo na suluhisho la matatizo yao na kwa gharama watakazomudu halafu buuuum una biashara kubwa na itakayokuletea mafanikio.

Mteja hajui anachotaka ila anatatizo ambalo anataka litatuliwe. Jua tatizo hilo na tayari una biashara.

SOMA; Vitu VIWILI Ambavyo Tayari Unavyo Na Vinavyoweza Kukufikisha Popote Unapotaka KWENDA.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.