KARIBU KWENYE SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA MWAKA 2015.

AMKA CONSULTANTS imekuandalia semina ya mafanikio kwenye biashara mwaka 2015. Katika semina hii utajifunz amambo yote muhimu yatakayokuwezesha kuanza, kukuza na kufikia mafanikio kwenye biashara yako. Semina itaanza tarehe 04/05/2015 na itaendeshwa kwa mwezi mzima kwa njia ya mtandao(yaani email). Mwisho wa kujiunga na semina hii ni tarehe 01/05/2015. Wahi sasa kujiunga ili upate maarifa yatakayokuwezesha kufanikiwa kwenye biashara. Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kujiunga bonyeza maandishi haya.

Biashara inafanana sana na siasa. Kwa sababu kitu kikubwa unachohitaji kwenye siasa na kwenye biashara ni ushawishi. Uweze kuwashawishi watu wanunue kwako na sio kwa mtu mwingine ambaye anauza kile ambacho wewe unauza. Kama ambavyo mwanasiasa anawashawishi watu wampigie kura yeye au chama chake na sio mgombea mwingine.

Lakini njia ya ushawishi kwenye biashara na siasa inatofautiana sana. Kwenye siasa, watu wanaweza kushawishi kwa hoja, ila kwa kuwa mpinzani naye anaweza kuwa na hoja nzuri, kinachobakia ni kumsema vibaya mpinzani. Kuonesha mapungufu yake na kwa nini hafai.

SOMA; Kama Unachofanya Huwezi Kufanya Miaka 50 Acha..

Sasa usijaribu hata kidogo kutumia njia hii kwenye biashara, ukifikiri ndio wateja watakuamini zaidi wewe, watamwona mshindani wako hafai. Wewe kuwa “bize” na biashara yako, mshawishi mteja wako kwa nini anunue kwako na kwa nini aendelee kununua kwako na sio kw amtu mwingine.

Mteja akikuuliza vipi kuhusu mtu X na huyu X ndio mshindani wako wa kibiashara, mwambie nafikiri anafanya biashara nzuri, ila sijajua kwa undani ni vitu gani vizuri anavyotoa. Najua hapa utaniambia sio, unataka kumwambia mteja sisi tunatoa hiki, wao hawatoi. Sisi tumeanisha hiki, wao wametuiga. Usijisumbue kufanya hivyo, acha mteja afanye kazi hiyo mwenyewe.

Kama akienda kwa mshindani wako na akakosa mambo mazuri aliyokuwa anayapata kwako unafikiri atafanya nini? Lazima arudi kwako. Hivyo kazana kuwa bora zaidi ya mtu mwingine yeyote anayefanya unachofanya wewe. Na usipoteze muda wako kuonesha kwamba mwingine hawezi kile unachoweza wewe, acha hii iwe kazi ya mtumiaji, mteja.

SOMA; Watu Hawa Wanakurudisha Nyuma Wajue na Uwaepuke.

Kumbuka tofauti ya biashara na siasa, biashara ni mahusiano endelevu, ya kila siku na kila wakati. Wakati siasa ni mahusiano ya kukatika katika, kila baada ya miaka kadhaa ndio mahusiano yanakuwa mazuri, baada ya hapo mtasubiri tena. Kwa nchi yetu ni kila baada ya miaka mitano. Tengeneza mahusiano mazuri kwenye biashara yako na toa kilicho bora, halafu huna haja ya kujali nini kitakachotokea, maana kitakuw abora.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.