Kuna baadhi ya biashara huwa zinakwenda na misimu fulani. Kuna kipindi watu wanakuwa wanazungumzia sana biashara ya aina fulani, inapata umaarufu sana na kila mtu anakimbilia kuifanya.
Hizi ni zile hadithi kwamba biashara fulani inalipa sana, ona watu fulani wamefanya na wamepata faida kubwa. Au kilimo fulani kinalipa sana, ona hawa wakulima walivyopata faida.
SOMA; Usimseme Vibaya Mshindani Wako Mbele Ya Mteja Wako.
Ni kweli biashara hizo zinakuwa zinalipa sana ila usichokijua ni kwamba, mpaka unazisikia taarifa hizo wewe, ina maana kuna wengi wameshafaidika zaidi. Yaani pale unaposikia taarifa kwamba biashara fulani inalipa sana, tayari umeshachelewa. Kuna wenzako wameshafaidika sasa. Na pale unapoingia wewe, kwa sababu mnaingia wengi mnashindwa kufaidika kama wale wa mwanzo. Hili si linatokea kila siku? Ni mara ngapi umejaribu biashara ambayo ulisikia inalipa ila ulipoingia ukajuta hata kuijua?
Ulisikia boda boda inalipa, ukanunua, ila changamoto uliyoipata unatamani hata kuigawa bure, au huenda umeshaachana nayo kabisa. Hapa wale waliokuambia inalipa, wao walishavuna zamani, nyinyi mnaokuja mwishoni na mnakuja wengi ndio mnakuja kuumia.
Ufanyeje sasa?
Lengo la kukushirikisha hili sio uogope kuingia wkenye biashara na sio uache kuingia wkenye biashara maarifu ila ujipange pale unapoingia kwenye biashara.
1. Usiingie kwenye biashara kwa sababu umeambiwa inalipa. ingia kwa sababu ndio kitu ambacho unapenda kufanya na upo tayari kuweka juhudi hata unapokutana na changamoto.
SOMA; Hii Ndio Sifa Muhimu Ya Mtu Unayetakiwa Kumuajiri.
2. Kuwa mdadisi na angalia soko ambalo halijafikiwa, weka mipango ya kulifikia. Hata kama watu hawasemi biashara hiyo inalipa, haimaanishi hakuna soko. Fanya uchunguzi wako kulingana na biashara unayofanya.
3. Jaribu vitu ambavyo havijawahi kufanywa. Ndio kuna hatari ya kupata hasara. Ila ukifanikiwa wewe ndio utakuwa mfungua njia, na wengine wengi watakimbilia huko kwa kusikia inalipa sana na wataendelea kukunufaisha wewe zaidi.
4. Usichukue ushauri wa biashara kwa kila mtu, au ushauri ambao kila mtu anaweza kutoa. Kwamba biashara fulani inalipa na wewe unakwenda kuifanya, angalau anayekuambia inalipa akuoneshe imemlipaje yeye, na sio kutumia maneno yanayozunguka mtaani.
5. Weka juhudi na maarifa, jifunze kila siku na jua sana biashara unayoifanya, kuna fursa nyingi ambazo mpaka sasa bado hujazitumia kupitia biashara hiyo.
SOMA; Ushauri Muhimu Kwa Waandishi Wa Blog; Idadi Sahihi Ya Wasomaji Unaohitaji Ili Kufanya Biashara.
Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.
Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.
KARIBU KWENYE SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA MWAKA 2015.
AMKA CONSULTANTS imekuandalia semina ya mafanikio kwenye biashara mwaka 2015. Katika semina hii utajifunz amambo yote muhimu yatakayokuwezesha kuanza, kukuza na kufikia mafanikio kwenye biashara yako. Semina itaanza tarehe 04/05/2015 na itaendeshwa kwa mwezi mzima kwa njia ya mtandao(yaani email). Mwisho wa kujiunga na semina hii ni tarehe 01/05/2015. Wahi sasa kujiunga ili upate maarifa yatakayokuwezesha kufanikiwa kwenye biashara. Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kujiunga bonyeza maandishi haya.