Uliisoma na kuielewa vizuri sheria ya mara mbili mara tatu? Kama hukuisoma ni muhimu sana wewe kufanya hivyo kwa sababu itakusaidia sana kwenye mipango yako ya muda na fedha kwenye biashara unayofanya. Unaweza kuisoma hapa; Tumia Sheria Ya Mara 2, Mara 3 Kwenye Mipango Yako Ya Biashara.
Leo nakupa sheria nyingine muhimu na hii itaangalia sana kwenye upande wa mipango yako ya faida na wateja. Kila mfanyabiashara anapanga kiasi gani cha faida anataka kutengeneza kupitia biashara hiyo. Na pia anapanga kiasi gani cha wateja ambacho anahitaji ili kupata faida hiyo. Je wewe huwa unatumia kigezo gani kuhakikisha unapata wateja hao unaohitaji?
Njia yoyote utakayotumia kufikia idadi ya wateja au kiasi cha faida itategemea mpango unaoanza nazo.
SOMA; Kama Unataka Maisha Yako Yawe Bora Na Yenye Mafanikio, Acha Kufanya Kitu Hiki Kimoja.
Kama unataka kupata wateja kumi, kuweka mipango ya kupata wateja kumi haitakupatia wateja kumi. Uatapata wachache zaidi ya hao uliopanga. Ili kuhakikisha unapata idadi hiyo ya wateja zidisha mara kumi. Kwa mfano kama unataka kufikia wateja kumi, kwenye mipango yako, weka wateja 100. Jiulize unawezaje kufikia wateja mia moja? Njia yoyote utakayotumia, hutafikia wateja 100 ila pia watakuwa wengi kuliko wale 10.
Ni sheria hii rahisi, hakuna kitu unachopoteza na unafikia malengo yako ya awali na hata kuyapita.
SOMA; Mambo Muhimu Ya Kuzingati Ili Kupata Mbegu Bora Kwenye Kilimo.
Anza kutumia sheria hii kwenye mipango yako ya kibiashara, na utaona unafikiria nje ya ukomo ambao umekuwa unajiwekea.
Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.
Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.
KARIBU KWENYE SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA MWAKA 2015.
AMKA CONSULTANTS imekuandalia semina ya mafanikio kwenye biashara mwaka 2015. Katika semina hii utajifunz amambo yote muhimu yatakayokuwezesha kuanza, kukuza na kufikia mafanikio kwenye biashara yako. Semina itaanza tarehe 04/05/2015 na itaendeshwa kwa mwezi mzima kwa njia ya mtandao(yaani email). Mwisho wa kujiunga na semina hii ni tarehe 01/05/2015. Wahi sasa kujiunga ili upate maarifa yatakayokuwezesha kufanikiwa kwenye biashara. Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kujiunga bonyeza maandishi haya.