Lengo la biashara ni kutengeneza wateja ambao watakuwa wanakuamini na mtaendelea kufanya biashara pamoja. Wateja hawa watakuw atayari kuwaambia watu wengine kuhusiana na biashara yako na hivyo kuleta wateja wengi zaidi.

Lakini sio wateja wote ni sawa na wote hawapatikani kwa njia moja rahisi. Kuna wateja ambao unaweza kuwapata kirahisi na kuna wengine unahitaji kuwa na mbinu nzuri ndio uweze kuwashawishi kuwa wateja wako.

SOMA; USHAURI; Jinsi Unavyoweza Kuondokana Na Changamoto Za Kuendesha Biashara Na Kuweza Kufikia Mafanikio Makubwa

Kama umeanzisha biashara na wateja wako ni watu ambao ulikuwa unafahamiana nao kabla hujaanza biashara yenyewe, bado huna biashara. Namaanisha hapa umekuwa kwenye biashara ila hujawez akutengeneza mteja mpya tofauti na wale watu ambao wanakujua wewe moja kwa moja. Sio vibaya kuwa na wateja ambao wanakufahamu, ila huenda wengi wao wanafanya baishara na wewe kwa sababu hawataki kukuangusha, kwa sababu utawaonaje kama watakwend akufanya biashara na watu wengine.

Sasa wewe huhitaji kujenga wateja kw anjia ya huruma. Unahitaji kujenga wateja wanaoridhishwa na kile unachotoa na hivyo kuwa tayari kuendelea kufanya biashara na wewe na hata kuwaambia watu wengine kuhusiana na biashara yako.

SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.

Biashara nyingi za huduma, kama huduma za ushauri, huanza na watu ambao unafahamiana nao, labda mmewahi kufanya kazi pamoja au mnajuana kwa muda mrefu. Ni vizuri kuwa na pa kuanzia ila usiridhike na kuona tayari umeshinda. Kazana kutengeneza wateja wengine ambao hukuwahi kufahamiana nao hapo awali. Hawa ni wateja ambao umewauzia sera zako kulingana na huduma unazotoa na wakashawishika kujaribu na wewe ukawapatia huduma bora ambayo hawakuwahi kuipata sehemu nyingine yoyote.

Kama biashara yako haijatengeneza mteja nje ya watu uliokuwa unawajua kabla hujaanza biashara, HUNA BIASHARA.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.

KARIBU KWENYE SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA MWAKA 2015.

AMKA CONSULTANTS imekuandalia semina ya mafanikio kwenye biashara mwaka 2015. Katika semina hii utajifunz amambo yote muhimu yatakayokuwezesha kuanza, kukuza na kufikia mafanikio kwenye biashara yako. Semina itaanza tarehe 04/05/2015 na itaendeshwa kwa mwezi mzima kwa njia ya mtandao(yaani email). Mwisho wa kujiunga na semina hii ni tarehe 01/05/2015. Wahi sasa kujiunga ili upate maarifa yatakayokuwezesha kufanikiwa kwenye biashara. Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kujiunga bonyeza maandishi haya.