Kwenye biashara unayofanya, kuna wateja ambao unajua kabisa wanaweza kunufaika na biashara yako, ila mpaka sasa hawanunui kwako. Je umewahi kujiuliza ni kwa nini? Kama bado unapoteza wateja wengi sana, hao unaowajua tayari na hata ambao bado hujawajua.
Kwenye biashara, kama ilivyo kwenye maisha ya kawaida, hakuna kitu kinachotokea kw abahati mbaya. Kila kitu kinatokea kwa sababu, kuna kitu kinasababisha kitu fulani kitokee.
SOMA; Usitegemee Nyundo Tu, Kuna Zana Nyingine Pia.
Sasa tuje kwa wateja ambao hawanunui kwako, ni kwmaba hawanunui kwako kwa sababu fulani. Ambayo wewe unatakiwa kuijua ili ujue jinsi gani unaweza kuondokana nayo ili upate wateja wengi na biashara yako ikue sana. Kuna sababu nyingi za kwa nini wateja hawanunui kwako, hapa nitakupa mbili, halafu wewe ongeza nyingine tatu kulingana na biashara unayoifanya. Kama utashindwa kuzipata, tuwasiliane ili tuweze kuziibua sababu hizo.
Sababu ya kwanza watu hawajui kama unafanya biashara wanayoitaka wao. Hii ni sababu rahisi sana kuiona lakini wengi hawaioni. Huwa tunafikiri watu wanajua kila kitu tunachofanya, sio kweli na hata kama wanajua bado wana mambo mengi ya kuwafanya wahofu kuliko kufikiria kuhusu baishara yako. Hivyo wakumbushe mara kwa mara kuhusu biashara yako. Fanya hivi kwa kutangaza na kujenga mawasiliano mengine na wateja wako.
SOMA; Njia KUMI Za Kubana Matumizi Yako Mwaka Huu 2015.
Sababu ya pili; wanapata huduma nzuri kwa mtu mwingine kuliko wanavyoweza kupata kwako. Ni jukumu lako kujua huduma hizo bora wanazopata na wewe kuziboresha zaidi na hakuna kitakachowazuia kuja kwako. Pia jenga nao mahusiano mazuri na wakuone wewe ni rafiki kwao na sio mtu unayeangalia tu fedha zao.
Ongeza mengine matatu yanayowazuia wateja kuja kwako, na yafanyie mambo hayo matano kazi. Usiache kunijulisha jinsi biashara yako imebadilika kupitia mbinu hizi tunazopeana kila siku. Na kama utashindwa kuyaibua mambo hayo mengine matatu, karibu tusaidiane kuyaibua.
SOMA; Haya Ndio Magonjwa Hatari Kwa Kilimo Cha Bustani.
Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.
Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.