Biashara mpya zimekuwa na mambo mengi sana. Kuna biashara ambazo huwa zinaanza kwa wateja wachache sana na kuna nyingine zinaanza na wateja wengi sana. Biashara zinazoanza na wateja wachache tulishajadili hapa na hatua gani za kuchukua. Kama hukupata nafasi ya kusoma makala ile isome hapa; Aina Tatu Za Wateja Na Jinsi Unavyoweza Kufaidika Nao.

Leo tutaangalia biashara ambazo zinaanza na wateja wengi ila baada ya muda wateja wote wanakimbia. Ili tuweze kuelewa vizuri changamoto tunayoijadili hapa, tuchukulie mfano wa biashara ya starehe na sana sana baa. Baa mpya inapofunguliwa na ikawa ni nzuri, mwanzo huwa na wateja wengi sana. Inaweza kuwa na wateja mpaka wengine wakakosa sehemu za kukaa ila wakawa tayari kusimama na vinywaji vyao. Na wakati huo kunaweza kuwa na baa ya jirani tu na eneo hilo ambayo ina wateja wachache sana na viti ningi viko tupu.

Kwa mtu asiyeelewa anaweza kusema kwamba mwenye baa inayojaza watu mpaka wakasimama anatumia dawa. Sio kweli, kuna kitu kimoja muhimu ambacho watu wanakitafuta na ndio maana watu wanakuwa radhi kukusanyika kwenye baa moja ambayo ni mpya.

SOMA; Tofauti ya mtazamo Kati ya Mtu wa Hali ya kati na Mtu wa hali Juu.

Baa mpya inapoanzishwa na ikawa ni nzuri, taarifa huwa zinasambaa kwamba kuna kiwanja kipya kimeanzishwa. Na pia baa hiyo inaweza kupewa sifa nyingi sana kitu ambacho kitawafanya watu wengi wasukumwe kwenda kujaribu sifa hizo ili nao wazifaidi. Pia watu wengine huenda tu kwenye baa kama hiyo ili nao wawe na kitu cha kuhadithia, kwamba na mimi nilishaenda sehemu fulani au kile ndio kiwanja changu.

Kwa mmiliki wa biashara kujua sababu hii inayowaleta watu, kutamsaidia sana kufanya watu hawa waendelee kuwa wateja wa kudumu. Kama atahakikisha watu wanaendele akupata kile walichosikia kinapatikana, na kuwafanya watu kujiona wao ni sehemu ya biashara hiyo kubwa anawafanya wateja kuendelea kuja mara kwa mara kwenye baa yake.

Lakini wenye baa hujisahau na kuanza kuendesha baa zao kwa mazoea na hivyo kushindwa kutoa ile huduma ambayo mteja alitarajia kuipata. Hii husababisha wateja kuanz akuihama baa hiyo na kama kuna nyingine imeanzishwa, basi wote wanahamia huko. Hapa napo watu watasema dawa zimeisha na mengine mengi.

SOMA; Ugumu Wa Mwanzo Mgumu…

Cheza na saikolojia ya watu, kila mtu ana njaa ya kitu fulani, ijue njaa ya wateja wako na ishibishe, utakimbia wateja.

Tumia mbinu hii kwenye biashara yoyote ambayo unaifanya na utatengeneza wateja wengi ambao mtakwenda pamoja.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.