Kama kuna maji ya makampuni matatu sokoni na maji ya kampuni moja yakawa yanauzwa kwa bei rahisi kuliko ya makampuni mengine, wateja watanunua yapi? Haihitaji elimu kubwa kujua kwamba watanunua yale maji yanayouzwa kwa bei rahisi. Wateja wengi watanunua maji hayo. Hii ni kwa sababu maji hayatofautiani sana, maji ni maji, tofauti ni majina na chupa zinazowekwa.
Lakini kwa maji hayo hayo mfanyabiashara mmoja anaweza kutengeneza hadithi ya ziada na kufanya watu wayanunue hata kama ni kwa bei kubwa kidogo. Kwa mfano kw ahapa Tanzania kuna maji ambayo yanaonekana ni ya kifahari zaidi na hivyo watu kuyaoenda na kuyanunua japo yana bei kubwa zaidi ya maji mengine. Ni maji sawa na ya kampuni nyingine ila yamejengewa hadithi na kuchukuliwa kama ndio maji namba moja.
SOMA; BIASHARA LEO; Tumia Kigezo Hiki Katika Bei Ili Uweze Kufanikiwa.
Hivyo unapoweka bei ya bidhaa au huduma zako angalia vitu hivi viwili.
1. Urahisi wa mteja kupata kitu hiko kwa bei ya chini kuliko unayoweka wewe. Kama upo kwenye biashara ya maji na wewe sio maji yanayoongoza basi una nafasi ndogo sana ya kupata wateja kama bei yako itakuw aya juu kuliko wengine. Jinsi ilivyo rahisi kwa mteja kupata huduma au bidhaa hiyo kwa bei rahisi zaidi ndivyo ilivyo ngumu kwako kufanikiwa kwneye biashara.
2. Hadithi unayotengeneza kwa bidhaa au huduma yako.
Je mtu anapotumia bidhaa au huduma yako anajisikiaje? Anajisikia yeye ni mtu muhimu au mtu wa pekee kwa kutumia bidhaa au huduma hiyo. Je anajiona wa hadhi ya juu kwa kutumia bidhaa/huduma hiyo? Na je ana uhakika kwmaba hiki ndio kitu kitakachotatua tatizo lake tofauti na vingine vinavyopatikana?
Lengo lako kwenye biashara lisiwe tu kushindana kwa kuweka bei ndogo, bali kutengeneza biashara ambayo itakuwa ya kipekee na itakayokuwezesha kutengeneza wateja wanaokuamini na watakaokuwezesha kufikia mafanikio makubwa.
SOMA; Unataka Kubaki Hapo Ulipo Au Unataka Kwenda Mbele?
Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.
Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.