Leo kaa chini na ujiulize na kupata jibu la swali lifuatalo;
Kama biashara yako isingekuwepo, je watu wanaokuzunguka wangekuwa katika hali gani? Je dunia ingekuwa kwenye hali gani?
Kama jibu ni hakuna tofauti kati ya kuwepo au kutokuwepo kwa biashara yako, basi huna biashara, yaani upo tu unasukuma siku.
SOMA; Tumia Kigezo Hiki Katika Bei Ili Uweze Kufanikiwa.
Swali lingine linalofanana na hilo na unalohitaji kujiuliza ni hili;
Ni kitu gani kitatokea kwa wateja wako kama utaacha kufanya biashara unayofanya sasa? Kama utafunga biashara yako, je wataona pengo lako? Je maisha yao yatakuwa hovyo ukilinganisha na yalivyo sasa?
Kama jibu ni hapana, basi una kazi kubwa ya kufanya kwenye biashara yako.
Kama kuwepo au kutokuwepo kwa biashara yako hakuleti tofauti yoyote kwenye jamii unayofanyia biashara au kwa wateja unaowahudumia, basi hujafanya kazi ya kutosha ya kutengeneza wateja ambao wanakuamini na wananufaika na biashara yako. Na hii ina maana kwamba kama akitokea mshindani mwenye mbinu nzuri anakunyanganya wateja wako wote na utajikuta kwneye wakati mgumu sana.
SOMA; Kitu Hiki Unachokilinda Ndio Adui Wa Mafanikio Yako.
Acha sasa kufanya biashara kwa hali ya hatari, acha kufanya biashara kwa sababu unataka faida tu. Anza kutengeneza maana kwa watu, anza kuacha alama kwenye maisha ya watu, anza kubadili na kuboresha maisha ya wateja wako na hakikisha jamii uliyopo na dunia wka ujumla inakuwa sehemu salama ya kuishi kutokana na biashara unayofanya.
Kama umekuwa unafuatilia kipengele hiki cha biashara leo, na kama utaendele kukifuatilia utakuwa umeshajifunza na pia utaendelea kujifunza jinsi ya kutengeneza wateja wanaokuamini na watakaowaleta wateja wengine na wengine zaidi. Kama bado una changamoto nipigie kwa namba ya simu iliyopo hapo chini.
Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.
Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.