Mafanikio ya biashara yako yatategemea wafanyakazi utakaokuwa nao kwenye biashara yako. Kwanza kama unafikiria kw anini uajiri, kama bado ni mfanyabiashara mdogo na unafanya kila kitu peke yako, ni muhimu sana kuandaa mpango wa kuajiri ili wakati wa kuajiri utakapofika usipate tabu. Jua majukumu unayohitaji kuyatoa kwa wengine ili biashara yako iweze kukua.

Unapokuw atayari kuajiri kwneye biashara yako, usichukue tu mtu yeyote kwa sababu amekuambia anaweza kufanya kazi, au kwa sababu ni ndugu yako, au kwa sababu anataka malipo kidogo. Lengo lako la kuajiri kwenye biashara ni kupata msaidizi ambaye ataiwezesha biashara yako kukua. Hivyo unahitaji kuwa makini sana kwenye zoezi hili.

SOMA; Hakuna Njia Ya Mkato…

Fuata hatua hizi katika kuajiri na utapata wafanyakazi bora watakaoiwezesha biashara yako kukua.

1. Jua majukumu ya mtu unayemuajiri na kile anachotakiwa kukamilisha.

2. Ajiri mtu ambaye ana uwezo wa kukamilsiha majukumu hayo. Usiajiri kwa sababu ya elimu, au kufahamiana, bali sifa ya mtu kwenye kuweza kujiongoza na kufanya majukumu yake kwa ubora wa hali ya juu.

3. Jadili majukumu ya mafanyakazi kwa pamoja, yaani wewe na mfanyakazi wako. Mwache apange majukumu yake mwenyewe ila aweze kutimiza majukumu unayotaka wewe kwenye biashara yako.

4. Mpe uhuru mfanyakazi wa kutekeleza majukumu yake na kuja na mawazo bora ya kuboresha kazi yake.

5. Toa mafunzo ya biashara na ya hamasa kwa nfanyakazi/wafanyakazi wako mara kwa mara. Hii itawasaidia kuweza kuwa na taarifa sahihi zitakazowawezesha kutekeleza majukumu yao vizuri.

Fuata hatua hizo, na kama ukihitaji msaada zaidi tuwasiliane.

SOMA; Kitu Muhimu Cha Kufanya Kabla Ya Kutumia Muda Au Fedha.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.