Moja ya changamoto kubwa zinazowazuia watu wengi kupata kile
wanachotaka, kufikia mafanikio wanayotarajia ni kuwa wapinzani wao wenyewe.
Yaani wewe unakuwa mpinzani wako mwenyewe. Bado hujaelewa inakuwaje?
Nitakufafanulia vizuri zaidi ili uweze kuelewa na kuchukua hatua pia.
Umekuwa unajifunza mambo mazuri na yatakayobadili maisha yako na
unakubali kabisa ya kwamba utakwenda kufanyia kazi yale ambayo umejifunza. Ila
unapoanza kuyafanyia kazi yale uliyojifunza yanaanza kukujia mawazo kwamba
unachofanya sio sahihi au hakiwezi kukuletea kile unachotaka.
Labda umejifunza kuhusu kuamka asubuhi na mapema ili ufanye
mambo yako ukiwa na utulivu. Unaamka siku ya kwanza na ya pili baada unaanza
kufikiria kwa nini nijitese, au ina maana gani, acha niendelee na muda wangu wa
kawaida wa kuamka.
Au umejifunza kutolalamika au kulaumu mtu yeyote yule, iwe
ndugu, serikali, bosi, bali wewe ni kuchukua hatua. Baadae unaona haiwezekani,
hawa watu ni lazima walaumiwe, wanafanya mambo ambayo sio. Unawalaumu,
unaridhika na maisha yako yanaendelea kuwa kama yalivyokuwa zamani.
SOMA; Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha
Yako.
Leo nikuambie kitu kimoja kwamba kuwa adui yako mwenyewe ni
kikwazo namba moja kwako kubadili maisha yako na kufikia mafanikio makubwa.
Unaweza kuwa na mawazo mazuri sana, unaweza kuwa na mipango mizuri sana ila kama
hutaacha kuwa adui yako mwenyewe, kama hutaacha kuwa mpinzani wako mwenyewe
hakuna kitakachobadilika kwenye maisha yako.
Safari ya kubadili maisha yako na kufikia mafanikio sio rahisi
kama unavyofikiri. Utapata upinzani mkubwa kuanzia ndani yako mwenyewe na hata
kwa wale wanaokuzunguka. Ukishafanya maamuzi ya kubadili maisha yako, komaa nayo
na usirudi tena nyuma, hata kama utajipa sababu nzuri kiasi gani.
TAMKO LA LEO;
Najua mara nyingi nimekuwa mpinzani wangu mwenyewe. Nimekuwa
napanga kubadili maisha yangu ili kufikia mafanikio lakini mimi mwenyewe naanza
kupinga vile nilivyopanga kufanya. Kuanzia leo naondoa kabisa upinzani mkubwa
ambao nimekuwa najiwekea mwenyewe. Nikishapanga kitu nitakomaa nacho mpaka
mwisho, mpaka nione kile ninachotarajia kuona.
Tukutane kwenye ukurasa wa 164 kesho, Like page yangu ya
Coach
Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha
kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.
TUPO PAMOJA.