Kupanga bei kwenye biashara ni changamoto kubwa sana unayotakiwa kuifanyia kazi vizuri kama kweli unataka kupata mafanikio makubwa kupitia biashara unayofanya. Watu wengi wamekuwa wakifikiria kwamba ukishusha bei basi utapata wateja wengi sana. Huu sio ukweli kuuza vitu kwa bei ya chini kunaweza kuwa kikwazo kwako kupata wateja wengi zaidi na hivyo kushindwa kufanikiwa.

Kwenye biashara ukiweka bei ya juu sana kuna wateja wengi watakuambia bei yako ni ghali na hatuwezi kuimudu lakini kuna ambao wataiweza pia. Ukiweka bei ya chini sana kuna wateja ambao watakuwa na shaka na thamani ya hiko kutu unachouza na hivyo kupata picha kwamba hata thamani yake ipo chini pia.

SOMA; Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.

Watu wengi wamekuwa wakipanga bei za biashara zao kwa vigezo vya juu juu sana bila ya kufikiria kwa kinakuhusu biashara zao. Wapo ambao wamekuwa wakifikiria kwa kuwa tukiweka bei juu watu wataona ni cha thamani, basi tuweke bei juu. Wanaweka bei juu na wanaendelea na biashara. Wengine wamekuwa wakifikiria kwa kuwa tukiweka bei chini watu wengi watakuja, basi wanaweka bei chini.

Katika hali hizi zote mbili, mfanyabiashara anamsahau kabisa mteja na kufanya mambo yake kwa upande wake yeye mwenyewe.

Leo nakushirikisha njia moja itakayokuwezesha kupanga bei inayomfaa mteja wako a yeye mwenyewe aridhike kwamba ni bei nzuri kwa thamani anayopata. Njia hii inaanza na wewe kujua thamani unayotoa na kisha kumjua mteja unayemlenga ni yupi. Kumjua hapa unahitaji kuwa na taarifa nyingi za mteja wako, ujue kipato chake, matatizo yake, vitu anavyopendelea na kadhalika. Kwa kujua taarifa hizi muhimu utaweka bei ambayo sio ya kuwafurahisha wengi, bali itakayojenga uhusiano mzuri na wateja wako.

SOMA; BIASHARA LEO; Umuhimu Wa Hadithi Ya Biashara Yako.

Unapojenga uhusiano mzuri, wateja wanakuamini na watawaleta wenzao ambao wana sifa kama za kwao na biashara yako itakwenda vizuri sana.

Usihangaike kuweka bei juu au bei chini, hangaika kuweka bei ambayo inaendana na mteja wako na jenga uhusiano mzuri na mteja huyu. Atakuwa chanzo kizuri cha ukuaji wa biashara yako.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.

Jiunge na COACHING/MENTORSHIP PROGRAM ambapo utapata muongozo wa hatua kwa hatua mpaka ufikie mafanikio kwenye kazi au biashara unayofanya. Bonyeza haya maandishi kupata maelekezo ya programu hii.