Kwanza kabisa kama ambavyo nimekuwa nasisitiza, usiwe kwenye biashara ambayo hujui mteja wako ni nani. Tafadhali sana, chukua muda wa kumjua mteja wako au achana na biashara hiyo. Humsaidii yeyote kwa kutojua mteja wa biashara yako, na biashara itakuwa ngumu sana kwako kama hujui mteja wako ni nani.

Sasa kikubwa baada ya kumjua mteja wako unatakiwa kujua vitu viwili muhimu kuhusu wateja wako.

Kitu cha kwanza ni nini wanahitaji. Mahitaji ni vitu vya msingi sana ambavyo kila mtu anatakiwa kuwa navyo ili maisha yake yaende vizuri. Kwa kukosa mahitaji maisha yatakuwa magumu sana. Watu watapigana kwa kila hali kuhakikisha wanapata mahitaji yao. Kama utajua mahitaji ya wateja wako na kujua njia bora ya kuyatimiza utakuwa na biashara ya uhakika na wateja ambao watakuamini na kukuletea wateja wengine wengi.

SOMA; BIASHARA LEO; Njia TANO Rahisi Za Kutangaza Biashara Yako.

Kitu cha pili kujua ni nini wanataka. Kuna vitu vingi ambavyo watu wanataka. Na vitu ambavyo watu wanataka sio muhimu sana na maisha yao hayawezi kukwama kwa kukosa vitu hivi wanavyotaka. Hivi ni vitu vya ziada ambavyo wangependa kuwa navyo kwenye maisha ila hata kama watavikosa bado maisha yataendelea kwenda.

Umuhimu mkubwa wa kujua mahitaji na matakwa ya wateja ni kwamba unapotafuta wateja lazima ujue jinsi ya kuwashawishi wafanye biashara na wewe. Kumfanya mtu anayehitaji kuwa mteja wako unatakiwa kumhakikishia kwamba utampatia mahitaji yake kwa gharama anazoweza kumudu na kwa huduma bora sana. Kumfanya mtu anayetaka kuwa mteja wako unatakiwa kumwonesha ni jinsi gani maisha yake yatakuwa bora zaidi ya yalivyo sasa kwa kutumia bidhaa au huduma unazotoa wewe.

Anayehitaji huna haja ya kumuonesha kwamba anahitaji ila anayetaka una kazi kubwa ya kumshawishi kwamba anatakiwa kufanya maamuzi kwa sababu yatakuwa bora kwake.

Fanyia kazi vitu hivi viwili kwenye biashara yako na utaona mabadiliko makubwa sana.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.

Jiunge na COACHING/MENTORSHIP PROGRAM ambapo utapata muongozo wa hatua kwa hatua mpaka ufikie mafanikio kwenye kazi au biashara unayofanya. Bonyeza haya maandishi kupata maelekezo ya programu hii.