wanafunzi wote waufanye, atakayepata maksi nyingi ndio amefaulu, atakayepata
chache amefeli.
Kuna watu pia wamekaa wakakubaliana kwamba ukiwa na magari ya
kifahari, ukawa na nyumba ya kifahari na fedha isipokuwa tatizo kwako basi wewe
umefanikiwa.
Vyote hivi vinaweza kuwa vipimo kwa sababu vitakusukuma na wewe
uweze kufika mbali zaidi ila sio vipimo sahihi kwa mafanikio yako. Hivi ni
vipimo vibovu sana kwako kujipima kama umefikia mafanikio au la.
Hakuna kipimo kimoja kinachoweza kupima mafanikio ya watu wote
kwa kigezo kimoja, ndio maana mara zote nimekuwa nakusisitizia sana
usijilinganishe na wengine. Ni vizuri kujua wengine wanafanya nini, ila usijione
umeshinda au umeshindwa kwa sababu ya kile unachofanya unavyokilinganisha na
wengine wanavyofanya.
Kwa kifupi ni kwamba usipime mafanikio yako kwa vigezo ambavyo
vimewekwa na watu wengine. Utakuwa hujitendei haki na kinaweza kuwa kikwazo
kikubwa sana kwako kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Sasa ujipime na nini?
1. Jipimie kwa malengo makubwa uliyojiwekea? Je umeyafikia? Na
kama hujayafikia ni kwa nini na umejifunza nini? Hakikisha malengo hayo ni
makubwa; soma hapa kujua umuhimu wa malengo makubwa; Ni
Bora Kuweka Malengo Makubwa Na Kushindwa Kuliko Kuweka Malengo Madogo Na
Kushinda.
2. Jipime kwa juhudi unazoweka, je ni juhudi za kutosha? Je
zinaleta matunda unayotarajia?
3. Jipime kwa ulivyokuwa jana na utakavyokuwa leo. je leo uko
bora zaidi ya ulivyokuwa jana? Je kadiri siku zinavyokwenda unazidi kuwa bora au
unazidi kuwa hovyo?
4. Jipime kwa maisha ya wengine uliyogusa. Je ni kwa kiasi gani
watu wengine wamenufaika kwa kile ambacho unafanya? Je wataendelea kunufaika na
kile unachofanya? Je watakukumbuka hata usipokuwepo?
Hivi ni baadhi ya vigezo sahihi kwako kujipima kama kweli
umefikia mafanikio au la. Vigezo vinavyotengenezwa na wengine ni sumu kwako,
usijaribu kuvitumia.
TAMKO LA LEO;
Nimekuwa napima mafanikio yangu kwa vigezo ambavyo vimewekwa na
watu wengine. Njia hii imekuwa inaniumiza na kunirudisha nyuma. Kuanzia sasa
nitapima mafanikio yangu kwa vigezo vyangu mwenyewe na nitahakikisha navifikia
na kuweka vikubwa zaidi ili kila siku niwe bora zaidi ya siku
iliyopita.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita
Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi
yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.
TUPO PAMOJA.