Ni vigumu sana kuweza kufanikiwa kwenye biashara, ndio kwa hiyo
unahitaji kujipanga vizuri na kutokukata tamaa ili uweze kufikia mafanikio
unayotarajia.

Umri wangu ni mdogo/mkubwa sana kuweza kuanza kufanya jambo hili
sasa. Ndio kwa hiyo unahitaji kuwa wa tofauti, licha ya umri wako kuwa
usiotegemewa bado unaweza kuweka juhudi na ukafikia kile ambacho unataka.

Nimejaribu mara nyingi sana lakini nimeshindwa. Ndio kwa hiyo
unahitaji kubadili mbinu zako, kuendelea kufanya kitu kile kile na kutegemea
majibu tofauti ni ujinga wa kupindukia.

Napenda sana kuanza biashara ila sina mtaji. Ndio kwa hiyo
unahitaji kufikiria njia ya kuweza kuanza biashara kidogo au kutafuta kitu
kingine cha kukuingizia kipato kwa sasa ili ujiandae na kuingia kwenye biashara
unaotazamia.

SOMA; Vitu Ambavyo Ni Rahisi Kufanya…. Na Madhara Yake.

Ukweli ni kwamba mtu yeyote anaweza kuja na sababu zaidi ya elfu
moja kwa nini hawezi kufanya kitu fulani. Ila sababu hizi haziwezi kusaidia
chochote.

Watu waliofanikiwa wanakuja na sababu lakini huzipatia sababu
zao suluhisho ambalo hulifanyia kazi na hatimaye kufanikiwa.

Usiwe mtu wa kutafuta au kutoa sababu tu. Hebu anza kuzipa
sababu zako suluhisho na utaona fursa nyingi sana za kukufikisha kwenye kile
unachotaka.

Wakati wowote unapokuja na sababu tafadhali sana mbele yake
ongeza NDIO KWA HIYO….

TAMKO LA LEO;

Najua sababu yoyote ninayojipa haiwezi kunifikisha kule
ninakotaka kwenda. Ila ninapoifanyia kazi sababu ninayoipata ndio natoa nafasi
kubwa kwangu kuweza kupata kile ninachotaka. Najua mjinga yeyote anaweza kuja na
sababu kwa nini hafanikiwi na hii ndio inazidi kumfanya asifanikiwe. Lakini mimi
sio mmoja wa wajinga hawa, kila sababu ninayopata lazima niipatie
ufumbuzi.

Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita
Amani
uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi
yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.

TUPO PAMOJA.