Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakipoteza wateja kwa kushindwa kufanya kitu rahisi sana, kutoa chaguo mbadala kwa wateja wako.

Kwa mfano mteja amekuja anataka kitu fulani ambacho wewe huna, badala ya kumwambia tu mimi sina hicho na aondoke, unaweza kumwambia sina hicho unachotaka ila kuna hiki kingine ambacho kinafanya kazi sawa na hicho na ni bora zaidi. Kwa kufanya hivi unaweza kumshawishi mteja kununua kitu hicho kingine.

Mara nyingi wateja wanakuwa wananunua kwa mazoea hivyo huenda hajawahi kujua kuna kitu kingine anachoweza kutumia kwenye hitaji lake na kilicho bora sana. Kwa wewe kutoa chaguo mbadala unamsaidia mteja na pia unatengeneza mteja.

SOMA; Sheria Tatu Muhimu Za Kufanikiwa Kwenye Maisha.

Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye kutoa chaguo mbadala.

Kuna wafanyabiashara wengi huwa wanatoa chaguo mbadala ila kwa kuwalaghai wateja ili tu wao wauze. Sasa wewe usiwe hivi maana unachotaka hapa ni kujenga wateja wanaokuamini. Zingatia haya;

1. Hakikisha chaguo mbadala unalotoa litakidhi mahitaji ya mteja. Kama sio usitoe hata kama wewe utapata faida.

2. Sema ukweli, usitake kuongeza chumvi ili kumvutia mteja, mweleze ukweli ni kipi atapata kwenye chaguo mbadala na kipi ambacho hatapata.

Wewe mwenye biashara unapaswa kuijua vizuri biashara yako kuliko mteja. Wewe unahitaji kuwa mshauri mzuri wa wateja wako. Na unapokuwa unawapa ushauri mzuri na wa uhakika watakusikiliza na kukuamini zaidi.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.

Jiunge na COACHING/MENTORSHIP PROGRAM ambapo utapata muongozo wa hatua kwa hatua mpaka ufikie mafanikio kwenye kazi au biashara unayofanya. Bonyeza haya maandishi kupata maelekezo ya programu hii.