Kwanza kabisa nikiri kwamba mimi huwa napinga sana dhana ya
kushindana. Ndio kuna wakati ushindani unaonekana ni mzuri, lakini tatizo
linakuja kwamba ukishakuwa na akili ya kushindana ndio unadumaa.
Kama unakuwa na akili ya kushindana maana yake lengo lako kubwa
ni kuwazidi wengine. Kuwa wa kwanza, kuwa bora zaidi ya wengine.
Sasa tuseme labda unafanya biashara eneo ambalo watu wanafanya
biashara kwa mitindo ya kizamani. Mtu akipata faida kidogo siku moja kesho yake
analala, anaona amewini maisha. Na wewe ukawa unashindana nao, unafikiri utafika
wapi?
Au tuseme unafanya kazi kwenye eneo ambalo kila mtu anakazana
kununua gari na wewe ukawa na akili ya kushindana, unafikiri mafanikio yako
makubwa kwenye maisha yatakuwa nini. Ukishanunua gari bora zaidi ya wengine
tayari umekwisha. Utaonekana wewe ndio wewe na kile kiroho chako cha kushindana
kitafurahi, kitakufanya uone maisha umeyamaliza.
SOMA; Sheria Tatu Muhimu Za Kufanikiwa Kwenye Maisha.
Lengo lako sio kuwa zaidi ya wengine, kama unataka kufikia
mafanikio makubwa. Bali lengo lako ni wewe kuwa bora zaidi yako wewe mwenyewe.
Wewe kuwa bora kuliko wewe mwenyewe. Wewe kuwa mbele yako mwenyewe. Hii ina
maana kwamba leo uwe bora zaidi ya ulivyokuwa jana, leo ufanye kazi yako au
biashara yako kwa ubora zaidi kuliko ulivyokuwa unafanya siku zilizopita. Leo
upate kipato kikubwa zaidi ya ulichopata siku zilizopita. Leo upate mteja mpya
tofauti na uliokuwa nao zamani.
Hiki ndio unatakiwa kupigania, hiki ndio unatakiwa kufanya kila
siku. Na sio kuingia kwenye mbio za kundi na kujiingiza kwenye mashindano ambayo
hujui hata yanakupeleka wapi.
TAMKO LA LEO;
Najua kukazana kuwa bora zaidi ya wengine ni kupoteza muda wangu
na kujizuia kufikia mafanikio makubwa. Kuanzia sasa nitakazana kuwa bora zaidi
yangu mwenyewe, nitakazana kuwa mbele yangu mwenyewe, kwa sababu najua kuna
uwezo mkubwa uliopo ndani yangu ambao bado sijautumia. Nitahakikisha nautumia
sasa ili niweze kufika mbali zaidi ya hapa nilipo sasa.
Tukutane kwenye ukurasa wa 180 kesho, Like page yangu ya
Coach
Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha
kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.
TUPO PAMOJA.