Unapokuwa unahitaji kufanya maamuzi ambayo huenda ni magumu
kwenye kazi yako, biashara yako au hata maisha yako kwa ujumla, huwa unahitaji
kupata ushauri. Unaweza kupewa ushauri mzuri sana kutoka kwa watu mbalimbali
ambao unaweza kuwa unawaamini sana.

Pamoja na ushauri huu muhimu bado wewe mwenyewe ndio utahitaji
kufanya maamuzi ya mwisho. Wewe ndio utakayekaa chini na kufanya maamuzi ambayo
utakuwa tayari kuishi nayo.

Hivyo ni muhimu sana wewe uwe na uwezo wa kufanya maamuzi.
Huwezi kutegemea tu watu watakavyokushauri, kwa sababu watu mbalimbali watakuwa
na ushauri tofauti. Kama hutakuwa na uwezo mzuri wa kufanya maamuzi ambayo
utakuwa tayari kuishi nayo, utaishia kufanya maamuzi ambayo
yatakupoteza.

SOMA; Mambo Kumi(10) Unayotakiwa Kubadili Leo Ili Kufikia Mafanikio
Makubwa.

Nakumbuka siku sio nyingi rafiki yangu mmoja aliniomba ushauri
kuhusiana na maamuzi ya kibiashara aliyokuwa anataka kufanya. Nilimpa ushauri
wangu na mambo muhimu anayohitaji kuzingatia. Baadae alinipigia kuniambia kwamba
ameamua kufanya tofauti na nilivyomshauri. Nilistuka kidogo kwa sababu
alichokuwa anakwenda kufanya ni kosa kubwa sana ambalo mimi binafsi nimewahi
kufanya na likanigharimu na nimekuwa naona wengi wakifanya kosa hilo na
linawagharimu sana. Nilijaribu kumwelewesha, labda kama hakuwa amenielewa
vizuri, lakini alisisitiza kuendelea na kile alichopanga kufanya.

Nilijikumbusha kwamba yeye pekee ndio mwinye kufanya maamuzi ya
mwisho na hivyo nilimwambia kila la kheri kama ndio maamuzi ambayo yuko tayari
kuishi nayo. Siku chache baadae alinipigia na kuniambia hataendelea tena na
mpango ule, hapa nilichanganyikiwa zaidi na sikutaka hata kujua
zaidi.

Katika maisha yako jiandae kuweza kufanya mamauzi ambayo ni
sahihi kwako na sio ya kusukumwa na mtu au kitu chochote.

TAMKO LA LEO;

Najua ya kwamba nitapata ushauri kutoka kwa watu wengi. Najua
ushauri huu utakuwa mzuri sana, lakini mwisho wa siku ni mimi pekee
nitakayehitaji kufanya maamuzi ambayo ni sahihi kwangu na nitakuwa tayari kuishi
nayo. Kila siku nitajijenga ili niweze kufanya maamuzi ambayo yatakuwa bora
kwangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 181 kesho, Like page yangu ya
Coach
Makirita Amani
uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha
kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.

TUPO PAMOJA.