Nina mpango mzuri sana wa biashara, biashara hii itakuwa na wateja wengi na itatengeneza faida kubwa. Asante kwa mpango huo mzuri, lakini elewa kwamba mpango wa biashara sio biashara.

Unaweza kuandika vizuri sana kwenye karatasi zako mteja wako ni nani, yupo wapi na utawezaje kumfikia, lakini hii sio biashara. Sisemi usiandike vitu hivi muhimu ila nataka uelewe kwamba kuwa na mpango mzuri wa biashara sio biashara.

Kuwa na wazo zuri la biashara pia sio biashara. Unaweza kuwa na wazo zuri sana lakini unapofika sokoni ukakuta mambo ni tofauti na ulivyotarajia.

SOMA; Unacho Kila Unachohitaji Ili Kufanikiwa.

Kuwa na wateja ambao wanasema WATANUNUA pia sio biashara. Watu wanaweza kukuahidi mambo mengi sana, lakini inapofika kwenye utekelezaji ndipo changamoto zinapoanzia.

Kuwa na mteja ambaye analipa au ameshalipa hiyo ndiyo biashara. Na hata kama unataka kumwambia mtu una biashara, mwambie una wateja wangapi ambao wameshalipa.

Kwa nini tunahesabu biashara kwa wateja ambao wameshalipa? Kwa sababu kama mtu ameshawishika kulipa, basi kuna thamani ambayo unaitoa kwao na hapo ndio tunasema kweli una biashara.

Hivyo kama wewe ndio unaingia kwenye biashara chukua ushauri huu muhimu sana, anza kutafuta watu watakaolipia bidhaa au huduma unayotoa na hiki ndio kitakuwa kipimo kizuri kwako kama una biashara au la.

Hivi unakumbuka tulisema lengo la biashara sio kupata faida eh? Tulisema lengo kuu la biashara na ambalo litakuletea faida ni nini? Kama hukumbuki soma hapa;

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.

Jiunge na COACHING/MENTORSHIP PROGRAM ambapo utapata muongozo wa hatua kwa hatua mpaka ufikie mafanikio kwenye kazi au biashara unayofanya. Bonyeza haya maandishi kupata maelekezo ya programu hii.