Kama unataka kufanya jambo jipya, kama unataka kufanya jambo
tofauti na wengine walivyozoea kufanya, naweza nikakuhakikishia jambo moja, WATU
HAWATAKUAMINI.
Watu hawatakuamini kwamba unaweza kufanya jambo hilo. Watu
hawatakuamini kwamba kuna uwezekano wa jambo hilo kufanyika kwa tofauti. Na hapa
ndipo watu wengi hukata tamaa na kuamua kuacha. Na hivyo watu wale walioshindwa
kuwaamini mwanzo wanakuwa sahihi na wanazidi kupata nguvu ya kuwaambia wengine
kwamba hawawezi au haiwezekani.
Leo nataka nikuulize, je unajua unatakiwa kufanya nini pale
ambapo watu hawakuamini kwamba unaweza? Au umekuwa mtu wa kukatishwa tamaa mara
nyingi na wewe kukubali?
Sasa kuna kitu kimoja muhimu sana unachotakiwa kufanya pale
ambapo watu hawakuamini kama unaweza. JIAMINI WEWE MWENYEWE. Wewe ndio umekuja
na mawazo hayo uliyonayo, wewe ndiye ambaye umekuwa unafikiria usiku na mchana
jinsi unavyoweza kubadili hali ya mambo. Wewe ndiye uliyefikiria na kuona kuna
njia mbadala na ambayo inawezekana. Sasa kwa nini ukubali kumsikiliza mtu ambaye
amefikiria kwa upande mmoja tu wa kwamba vitu haviwezekani?
SOMA; Hukuja
Na Maelekezo Kwa Mtumiaji Na Kwa Nini Ufurahie Hili.
Kama utawasikiliza watu hawa utakuwa hujajitendea haki kabisa,
kwa sababu hata watu hawa sio kwamba wana uhakika haiwezekani, ni vile tu
hawajawahi kuona mtu mwingine akifanya hicho unachotarajia kufanya.
Kama watu hawaamini kwamba unaweza, huo ndio wakati wa kujiamini
na hata kufurahia sana kwenye maisha yako. Unajua ni kwa nini? Kwa sababu
unapoanza kufanya kitu ambacho wengi wanaona hakiwezekani, jua unafanya kitu
ambacho sio cha kawaida, unafanya kitu kikubwa. Na mafanikio yanakuja kwa
kufanya vitu ambavyo sio vya kawaida.
TAMKO LA LEO;
Najua ya kwamba pale ninapopanga kufanya jambo kubwa, watu wengi
watashindwa kuniamini. Huu ni wakati muhimu sana wa mimi mwenyewe kujiamini na
kuendelea kuweka juhudi. Hakuna mafanikio yanayokuja kwa kufanya vitu ambavyo ni
vya kawaida. Hivyo ninapoona watu hawaniamini kwa kitu kikubwa ninachotaka
kufanya, najua hapo ndio penye mafanikio.
Tukutane kwenye ukurasa wa 182 kesho, Like page yangu ya
Coach
Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha
kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.
TUPO PAMOJA.