Kuna jambo moja muhimu sana kwenye maisha ambalo unatakiwa kuwa
unalijua. Na sio kulijua tu bali kulifanyia kazi kila siku maana kwa jambo hili
moja ndio watu wanafanikiwa au wanashindwa.

Jambo hilo ni kwmaba, tabia mbaya ni rahisi sana kutengeneza ila
ni ngumu sana kuishi nazo. Na kwa upande wa pili, tabia nzuri ni ngumu sana
kutengeneza ila ni rahisi sana kuishi nazo. Hivyo ni wewe kuchagua kuwa tayari
kufanya kipi ili uweze kuishije baadae.

Urahisi wa kutengeneza tabia mbaya.

Tabia mbaya ni rahisi sana kutengeneza, kwa mfano ulevi, ni
rahisi sana kuwa mlevi, anza kunywa pombe kila siku na kunywa nyingi uwezavyo,
hata hivyo unasikia raha, hivyo ni rahisi kutengeneza. Ila sasa maisha ya ulevi
ni magumu sana, ni vigumu sana kuweza kufurahia maisha kama tayari wewe ni
mlevi, utajikuta maisha yako yametawaliwa na ulevi na unajiona kama huwezi
kutoka tena huko.

Tabia zote mbaya, iwe ni uvivu, wizi, uongo, kula hovyo zote ni
rahisi sana kutekeleza. Ila kuishi nazo baada ya kuwa zimejijenga ni vigumu
sana.

SOMA; Kama Unataka Kumaliza Matatizo Yako Ya Fedha Fanya Kitu Hiki
Kimoja.


Ugumu wa kutengeneza tabia nzuri.

Kwa upande wa pili, tabia nzuri ni vigumu sana kuzitengeneza
lakini ukishakuwa nazo ni rahisi sana kuishi nazo. Kwa mfano tabia ya kujiwekea
akiba, ni vigumu sana mwanzoni, inabidi ujinyime inabidi uonekane huendi na
wakati na wakati mwingine utahitaji kuzishinda tamaa zako. Ila unapokuwa na
tabia hii ni rahisi na vizuri sana kuishi nayo kwa sababu unajua kuna akiba
ambayo inaendelea kukua na hivyo kuvutiwa kuweka zaidi.

Unahitaji nguvu ya ziada ili kuweza kufikia mafanikio, ingekuwa
rahisi kila mtu angekuwa nayo. Sio rahisi na ndio maana kuna wakati utaona kama
unajitesa, endelea hivyo hivyo na mambo yatakuwa mazuri sana.

TAMKO LA LEO;

Najua nina machanguo mawili, nipate raha ya muda mfupi sasa
halafu niteseke kwa muda mrefu au nipate shida ya muda mfupi sasa na kuishi kwa
raha muda mrefu. Mimi nimechagua kuteseka kwa muda mfupi sasa ili niishi kwa
raha muda mrefu ujao. Nitatengeneza tabia ambazo ni nzuri kwa sasa, ambazo ni
ngumu kutengeneza lakini najua baadae nitafurahia kuishi
nazo.

Tukutane kwenye ukurasa wa 183 kesho, Like page yangu ya
Coach
Makirita Amani
uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha
kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.

TUPO PAMOJA.