Nikimaliza kuandika hapa na mtu akasoma, bado ataniandikia kwamba anatafuta wazo la biashara. Yaani wazo la biashara limechukuliwa kama ni kitu kikubwa sana ambacho watu wanapigana nacho ili wakipate. Ni kama ukishapata wazo basi mambo yako yote yamenyooka.
Nimekuwa nikisema mara kwa mara mwamba wazo la biashara linaanza na wewe mwenyewe. Sio kwa kupewa au kwa kuuziwa. Kwa sababu wazo la biashara lina thamani ndogo sana kwa sasa, unahitaji kuja na wazo lako mwenyewe ili uwe tayari kulitolea jasho.
Sasa leo nakupa njia nyingine rahisi ya kupata wazo la biashara. Hivi unajua kwamba kila siku watu wamekuwa wakikupa wazo la biashara? Ndio kila siku watu wanakuja kwako na wanakupa wazo la biashara, ila kwa vile wewe hujafungua masikio yako ya ndani unashindwa kulisikia wazo hilo na hivyo linapita.
SOMA; Hakuna Kinachodumu Milele…
Sitaki maneno mengi hapa nikuambie tu hivi, angalia mara nyingi watu wanakuja kwako wakitaka uwasaidie nini. Kama hujawahi kufikiria hili anza leo. kila wakati ambapo mtu atakuja kukuomba kitu andika chini ni kitu gani amekuomba umsaidie au umfanyie. Fanya zoezi hili kwa wiki moja na utaona kuna kitu ambacho watu wengi wanakuomba.
Basi kitu hiki ndio unakiweza vizuri na wengi wanakuamini ndio maana wanakuomba msaada. Sasa anza biashara hapo kwa kutafuta mtu ambaye anaweza kukulipa wewe kwa kumpatia msaada huyo, kwa jina la kibiashara tunamuita mteja. Na hapo unakuwa umeanza biashara.
Au kama hiyo ni ngumu kufuatilia na upo kwenye mitandao ya kijamii, nenda kwenye mtandao wako wakijamii na andika hivi; HABARI ZA LEO MARAFIKI ZANGU. NAOMBA KUULIZA KAMA UNGEKUJA KWANGU UKIHITAJI NIKUSAIDIE AU KUKUSHAURI JAMBO MOJA TU, INGEKUWA KITU GANI? NAOMBA USIPITE BILA YA KUWEKA MAONI YAKO, NAHITAJI KUJUA ILI NIWEZE KUBORESHA ZAIDI KITU HIKO. (nakuruhusu ukopy na ukapest). Baada ya kuandika hayo angalia majibu ya marafiki zako, na utashangaa kuna kitu kimoja wengi wanakirudia sana, kifanyie kazi hiko na hapo tayari una biashara yako.
Wakati mwingine ukianza kulalamika unataka kufanya biashara ila huna wazo hakikisha umeshatumia njia zote hizo. Kama unahitaji msaada wa karibu zaidi tumia mawasiliano yangu hapo chini.
Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.
Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.
Jiunge na COACHING/MENTORSHIP PROGRAM ambapo utapata muongozo wa hatua kwa hatua mpaka ufikie mafanikio kwenye kazi au biashara unayofanya. Bonyeza haya maandishi kupata maelekezo ya programu hii.