Kwa mfano umeshakubaliana na mtu mtafanya kitu fulani halafu
dakika za mwisho anakuambia nimebadili mawazo, sitafanya tena kama
nilivyokuambia. Unajisikiaje? Unachukuliaje hali kama hiyo?

Labda ni biashara na umeshakubaliana na mteja ila baadae
anakuambia nimebadili mawazo. Au ni kwenye ajira na umeshakubaliana kitu fulani
na mwajiri wako, umeshajiandaa kabisa na anakuambia nimebadili mawazo, hutafanya
tena hivyo. Au ni kwenye maisha yako ya kawaida, ulipanga muoane na mtu na
dakika za mwisho anakuambia nimebadili mawazo? Au umeshaona na mtu na kati kati
ya safari anakuambia nimebadili mawazo?

Najua kama wewe ndio umeambiwa hivi unaweza kujisikia vibaya
sana. Unaweza kuona aliyebadili mawazo hafai na ameharibu maisha yako. Lakini
ukweli ni kwamba yeye ametumia haki yake ya msingi, kuruhusu mawazo yake
yamchagulie kile ambacho anaona ni bora kwake. Hakuna jinsi unaweza kuzuia
hilo.

SOMA; Kabla Hujakubali Kila Unachoambiwa, Kumbuka Jambo Hili Moja Muhimu
Sana.


Badala ya wewe kulalamika kwamba kwa nini hakukwambia mapema au
kwa nini alikubali mwanzoni, furahi kwamba umejua mapema kabla hata hujapoteza
muda mwingi. Shukuru kwamba umejua ni mtu wa aina gani na jifunze wakati
mwingine kuangalia vitu muhimu kabla hujaingia kwenye makubaliano na mtu ambayo
ni muhimu.

Jipe ruhusa ya kubadili mawazo, wape wengine ruhusa ya kubadili
mawazo na usitake kuishi maisha ya kufungwa au kuwafunga wengine kwa sababu tu
wanaogopa kubadili mawazo. Maisha yanapaswa kufurahiwa na sio kuishi kwa ajili
ya kuwaridhisha wengine.

TAMKO LA LEO;

Najua nina ruhusa ya kubadili mawazo hata kama nilishakubaliana
na mtu. Najua pia kwamba watu wana ruhusa ya kubadili mawazo yao hata kama
walishaniahidi kitu. Naheshimu uhuru wangu na wa kila mtu na ni kwa uhuru huu
ndio naweza kuishi maisha ninayoyafurahia na yenye faida kwa wengine
pia.

Tukutane kwenye ukurasa wa 185 kesho, Like page yangu ya
Coach
Makirita Amani
uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha
kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.

TUPO PAMOJA.