Kuna watu watatu ambao kwa wewe kujua au kutokujua wamekuwa
wanakuzuia kufikia mafanikio.

Sio kwamba wao wanakuja na kukuzuia wewe kufikia mafanikio, ila
kwa sababu yao wewe mwenyewe umeshindwa kufikia mafanikio kwenye maisha
yako.

Aina ya kwanza ya watu hawa ni watu ambao unataka kuwalinda.
Kuna watu ambao wewe unataka kuwalinda na hivyo unajizuia kufikia mafanikio ili
uendelee kuwalinda. Kuna baadhi ya watu wanaogopa kufikia mafanikio kwa sababu
wanataka kuendelea kuwa na watu wanaowazunguka. Kuna wafanyakazi ambao wanaogopa
kuonesha ubora wao kwenye kazi zao kwa sababu wanaogopwa kuchukiwa na wenzao au
kuonekana ni hatari kwa mabosi zao.

SOMA; Wajue Watu Hawa na Waepuke Kwenye Maisha Yako.

Aina ya pili ni watu ambao unajaribu kuwaadhibu. Kuna watu ambao
unaweza kuwa unataka kuwaadhibu na hivyo ukajizuia wewe kufikia mafanikio. Labda
wazazi wako hawakukupatia kile ulichofikiri kingekuwa bora kwako. Na hivyo
unataka uwaoneshe kwamba walikosea na hivyo wewe huwezi kufikia mafanikio kama
ya wengine…. kwa sababu ya kutojali kwao.

Aina ya tatu ni watu ambao unataka kuwafurahisha. Hawa ni watu
ambao unataka kuwafurahisha ili waendelee kukuona kama wanavyopenda kukuona na
hivyo kujizuia kufikia mafanikio. Kuna watu ambao wanalazimika kuvaa mavazi ya
bei ghali, kuendesha magari ya bei ghali na hata kuishi maeneo fulani ili tu
waonekane.

Wajue watu hawa watatu kwenye maisha yako na malizana nao,
hakikisha unaishi maisha uliyochagua wewe mwenyewe, yatakayokufikisha kwenye
mafanikio unayotaka na sio kuwalinda watu, kuwaadhibu au kuwafurahisha.

TAMKO LA LEO;

Nimeamua sasa kwamba sitaki tena kuwalinda watu, kuwaadhibu au
kuwafurahisha. Nahitaji kuishi maisha ambayo yatanipa furaha na kunifikisha
kwenye mafanikio na sio maisha ambayo yatanirudisha nyuma. Nitaweka juhudi na
maarifa ili niweze kuwa bora zaidi ya nilivyo sasa.

Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita
Amani
uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi
yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.

TUPO PAMOJA.