Siku ya leo kuna watu wengi sana watakaokuudhi. Kuna watu wengi
watakukasirisha na wengine watakufanya ujisikie vibaya sana. Kwa hasira
inayotokana na watu hawa unaweza kufanya maamuzi ambayo sio mazuri sana kwao na
kwako pia.
Ila kumbuka mara nyingi unapokuwa na hasira huwezi kufanya
maamuzi ambayo ni sahihi. Na hata kama mtu atakuchukiza kiasi gani, hata kama
atakuudhi kiasi gani kwa wewe kuwa na hasira, kwa wewe kuendelea kuwa na
kinyongo naye haimuumizi yeye bali inakuumiza wewe mwenyewe.
SOMA; JICHO KWA JICHO; Tutabaki Na Dunia Ya Vipofu.
Sasa leo nataka nikupe kitu kimoja muhimu cha kufanya kabla jua
halijazama. Hakikisha jua linapozama umemalizana na kitu hiki ili siku yako ya
kesho iwe bora sana.
Kabla jua halijazama leo hakikisha umewasamehe wote waliokukosea
leo. hakikisha umeondokana na vinyongo vyote ambavyo unaweza kuwa
umejitengenezea kwa siku ya leo. Acha mambo haya yote yazame na jua la leo, ili
jua linapochomoza kesho uanze siku yako ukiwa vizuri na uweze kufanya
makubwa.
Usikubali jua lizame ukiwa bado na hasira au kinyongo. Vitu hivi
havikusaidii chochote zaidi ya kufanya maisha yako kuwa magumu na hata kuharibu
afya yako.
TAMKO LA LEO;
Sitakubali siku ya leo na siku nyingine yoyote ipite nikiwa na
kinyongo au hasira kwenye moyo wangu. Jua litakapozama nitahakikisha nimeachia
yote niliyokumbana nayo siku ya leo. kama kuna mtu ameniudhi, amenikasirisha au
amefanya chochote ambacho kimenifanya niwe na kinyongo nitamsamehe. Maisha yangu
ni muhimu zaidi ya chuki ninazotaka kutengeneza na watu.
Tukutane kwenye ukurasa wa 188 kesho, Like page yangu ya
Coach
Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha
kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.
TUPO PAMOJA.