Swali muhimu sana hilo kujiuliza kama hujawahi kufanya hivyo.
Ngoja nikuulize tena vizuri ili twende sawa,

Je unalipwa mshahara kwa sababu unaonekana kazi au kwa sababu
una thamani unayotoa kwenye kazi yako?

Je mteja wa biashara yako ananunua kutoka kwako kwa sababu
amekuona na wewe unafanya biashara au kwa sababu kuna thamani anaifuata?

Jipe muda wa kujibu swali hili, maana ndio msingi wako wote wa
mafanikio umelala hapo.

Kulipwa kwa kuonekana.

Hapa ni pale unapotegemea malipo kwa sababu tu umeonekana
kazini, au kwa sababu tu na wewe unauza. Hivyo kinachotokea ni wewe kujionesha
kwamba na wewe upo. Kama ni kazini basi unahakikisha unaonekana una kazi nyingi
na upo bize kumbe hakuna thamani kubwa unayotengeneza. Ukiwa mtu wa aina hii
inakubidi uonekane una juhudi sana kumbe ukweli sio hivyo.

Kama ni biashara unakazana kutangaza ili uonekane na wewe
upo.

Tatizo la kutegemea kipato kwa njia hii ni kwamba huwezi kupata
kipato kizuri na huwezi kujiamini.

SOMA; Ukiendelea Na Maisha Haya Watu Watakunyanyasa Sana…

Kulipwa kwa kuongeza thamani.

Hiki ndio wanachofanya watu wote wenye mafanikio. Hawaendi
kazini ili waonekane na wao wamekuja, ila wanakwenda pale kuleta mabadiliko.
Kuongeza thamani kwenye kile wanachofanya na hivyo kuwanufaisha wengi
zaidi.

Kama ni wafanyabiashara wanakazana kutatua matatizo
yanayowasumbua wengi. Na kwa kuwa suluhisho lao ni bora watu wanakuwa
wanawatafuta wenyewe.

Na kwa upande wa kipato, watu hawa wao wenyewe ndio wanaamua
walipwe kiasi gani, wakitaka kuongezwa kipato wanaongeza thamani
wanayotoa.

Je umeshajua uko wapi? Kazana kuongeza thamani na sio kukazana
kuonekana. Unapokazana kuonekana maana yake unapiga kelele. Unapokazana kuongeza
thamani umuhimu wako pia unaongezeka. Na kila mtu atataka kufanya kazi na wewe.
Na utaanza kupanga ulipwe kiasi gani.

TAMKO LA LEO;

Najua njia bora ya kutengeneza kipato sio kwa kuonekana bali kwa
kuongeza thamani. Kuanzia sasa nitakuwa nakazana kuongeza thamani na sio
kuwapigia watu kelele ili wajue kama nipo. Najua nitakapotoa thamani kubwa na
kipato changu pia kitaongezeka.

Tukutane kwenye ukurasa wa 192 kesho, Like page yangu ya
Coach
Makirita Amani
uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha
kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.

TUPO PAMOJA.