Kuna watu ambao huwa wanaweka furaha kwenye kipimo. Mtu
anafikiri nikishapa kitu fulani basi nitakuwa na furaha sana.
Kwa hiyo huwa inaanza hivi;
Uko mtoto mdogo unatamani sana kwenda shule unasema nikianza
darasa la kwanza nitafurahi sana. Unaanza na unagundua hakuna kitu cha tofauti
sana.
Unaendelea na shule kwa miaka saba, unapokaribia mwisho
unasubiri kwa hamu sana ukisema nikimaliza darasa la saba tu, nitakuwa na raha
sana. Unamaliza na unaona kumbe kilikuwa kitu cha kawaida sana.
Unaanza sekondari unasoma na kufikiria nikimaliza tu, nitakuwa
na raha, unamaliza na maisha ni yale yale.
SOMA; Ndege Wa Angani Hawalimi Ila Wanakula, Kuna Mambo Haya Matano(5)
Pia Wanakuzidi Ujanja.
Hivyo hivyo mpaka unaingia chuoni, unafikiria nikimaliza na
nikapata kazi, maisha yangu yatakuwa ya furaha sana. Unamaliza na labda unapata
kazi na unakuta ni kawaida tu na huenda ukakutana na changamoto nyingi
zaidi.
Hivyo pia inakuwa kwenye kila kitu unachofanya kwenye maisha
yako, unafikiri ukipata kitu fulani utakuwa na furaha, ila unakifanya na
unagundua kuna kingine zaidi cha kufanya.
Ni vigumu sana kupima furaha kwa vipimo hivi hasa pale
unaposogeza kipimo kila unapokifikia.
Wakati sahihi kwako kuwa na furaha ni sasa hivi, hapo ulipo na
unaposoma hii. Na utakapotoka hapo kila wakati kuwa na furaha. Kama unafikiria
utaipataje furaha chukua kalamu na karatasi na andika vitu kumi unavyoshukuru
kuwa navyo hapo ulipo. Huenda ni kazi au biashara inayokupatia fedha za
kuendesha maisha, huenda ni familia inayokupenda, huenda ni marafiki mnaopendana
na kadhalika.
Huwezi kupima furaha na ukaipata, furaha ipo ndani yako, ni wewe
kuifikia na kuiishi.
TAMKO LA LEO;
Kuanzia sasa naacha kupima furaha kwa sababu nimegundua kwamba
kuweka kipimo kwenye furaha ni sababu namba moja ya kushindwa kuifurahia. Hapa
nilipo nina furaha kwa sababu nina vitu hivi vifuatavyo(soma orodha yako ya vitu
kumi).
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita
Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi
yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.
TUPO PAMOJA.