Ushabiki umekuwa kikwazo kwa watu wengi sana kuweza kufikia
mafanikio makubwa. Watu wamekuwa wakijikuta wanalazimika kuacha mambo yao ya
msingi kwa sababu hataki kupitwa na kitu ambacho anashabikia.

Kuna watu ambao ni mashabiki wa mpira kiasi kamba hawezi kuacha
kuangalia timu yake inacheza hata kama kutakuwa na kitu gani anachofanya. Kuna
wengine ni mashabiki wa muziki, mashabiki wa tamthilia, mashabiki wa matamasha
mbalimbali na pia mashabiki wa siasa.

Sina tatizo na wewe kuwa shabiki, ila kama kweli lengo lako ni
kuwa na maisha bora na yenye mafanikio basi unatakiwa kufikiria mara mbili
kuhusu ushabiki wako.

Fikiria kile unachoshabikia na jiulize, je kinakuongezea
maarifa? Je kinakuongezea kipato? Je kinafanya maisha yako na ya wengine kuwa
bora zaidi/ kama jibu ni hapana basi ushabiki huo usiwe kipaumbele kwenye maisha
yako.

SOMA; Huwezi Au Hutaki? Kabla Hujaniambia Huwezi, Hakikisha
Huponi.


Mimi nilikuwa mshabiki wa tamthilia mpaka siku moja mtu
akaniambia(kupitia kitabu nilichokuwa nasoma), unapoangalia tv, kuna mambo
mawili yanatokea. Yule unayemwona kwenye kioo cha tv analipwa kwa wewe
kumwangalia na wewe unalipa kumwangalia mtu huyo. Je unataka kuwa upande upi?
Kulipa uangalie maisha ya wengine au kulipwa kwa watu kuangalia maisha yako?
Kuanzia hapa nilikata shauri la kutoangalia tamthilia tena, sijaziangalia tangu
mwaka 2012 na hakuna nilichokosa zaidi ya maisha yangu kuwa bora zaidi.

Achana na ushabiki ambao hautaboresha maisha yako na anza leo
kuwa shabiki wako mwenyewe. Mimi ni shabiki namba moja wa Makirita Amani, huwa
sikosi chochote alichopanga kufanya na nitaahirisha vingine vyote ili
kuhakikisha namshabikia. Je shabiki wako namba moja ni nani?

Una muda mfupi sana kuanza kuugawa kwa kushabikia vitu ambavyo
havina msaada mkubwa kwenye maisha yako, hasa ambavyo unaweza kuvipata baadae.
Kwa mfano kama unashabikia timu ya mpira, badala ya kukesha ukiangalia mpira na
kesho yake ukashindwa kufanya kazi zako vizuri kwa nini usilale mapema na kesho
yake utayajua tu matokeo? Hakuna tofauti yoyote kuona magoli mawili yakifungwa
na kuja kuyaona kesho yake. Tena siku hizi mipira inarekodiwa kwa hiyo unaweza
kuangalia kwa muda wako.

Narudia tena, usikubali ushabiki uharibu ratiba zako, una mengi
yakufanya, yape kipaumbele.

TAMKO LA LEO;

Najua ushabiki wangu umekuwa unanifanya nishindwe kufikia
mafanikio makubwa. Nimekuwa nashabikia mambo mengi sana. Nimekuwa naahirisha
mipango yangu kwa sababu tu nisipitwe na ushabiki. Leo naamua kwamba mtu wa
kwanza kumshabikia ni mimi mwenyewe. Sitakatisha ratiba zangu kwa sababu kuna
kitu nakishabikia. Nitaendelea na mipango yangu na ninajua nitafahamishwa kila
kinachoendelea.

Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita
Amani
uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi
yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.

TUPO PAMOJA.