Wakati unaweka juhudi za ziada zaidi ya wengine hakuna
atakayekutukuza, na wengine wengi watakukatisha tamaa.
Wakati wewe unafanya kazi wakati wengine wamepumzika,
wanastareheka hakuna atakayekuwa anakumulika, na wanaojua watakuwa wanakubeza na
kukuona hujui unachofanya.

Kama utaendelea kung’ang’ana na kuweka juhudi licha ya watu
kukususa na wengine kukukatisha tamaa, unajua ni nini kitatokea?

Mambo yako yatakuwa mazuri, utaanza kupata majibu tofauti na
wengine wanayopata, kila mtu ataanza kuona mafanikio yako. Na wakati huu unajua
ni kitu gani kitatokea?

Kila mtu ataanza kukutukuza, kukusifu, huyu hakukata tamaa. Na
wanaokujua wataanza kusema tulijua tu atafika mbali, wakati hakuna hata siku
moja wamekutia moyo.

Je utawachukia watu hawa kwa sababu ni wanafiki, wanakusifia
wakati tu umefikia mafanikio? Hapana usifanye hivyo, sio kosa lao, ndivyo dunia
ilivyowatengeneza. Dunia inapenda washindi, dunia haina muda na wanaoteseka,
wanaokazana na ukishindwa ndio kabisa utakuwa mfano wa kuwatisha wengine.

Ufanye nini sasa? Endelea kuweka juhudi, endelea kushinda. Hata
pale wanapokusifia usione ndio umefika mwisho, wacha wao waendelee kutoa sifa,
na wewe endelea kuweka juhudi.

TAMKO LA LEO;

Najua dunia inapenda washindi. Hainisumbui kama sasa hivi hakuna
anayeniona pamoja na juhudi kubwa ninazoweka. Na hata nitakapofikia mafanikio na
waliokuwa wa kwanza kunicheka wakawa ndio wa kwanza kusema walijua nitafanikiwa
pia halitakuwa tatizo kwangu. Mimi nitaendelea kuweka juhudi bila ya kujali watu
wanasema nini.

Tukutane kwenye ukurasa wa 196 kesho, Like page yangu ya
Coach
Makirita Amani
uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha
kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.

TUPO PAMOJA.