Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu THE POWER OF NO.

Habari ndugu msomaji wa makala za uchambuzi wa Mambo 20 kutoka kwenye kitabu cha wiki. Karibu kwenye mfululizo wa makala zetu za kila wiki. Wiki hii tutaangazia kitabu kinachoitwa The Power of NO. Kitabu hichi kimeandikwa na moja wa waandishi wazuri sana wa vitabu aitwaye James ALTUCHER akishirikiana na mkewe aitwaye CLAUDIA ALTUCHER. Mwandishi anazungumzia nguvu ya kusema HAPANA katika Nyanja mbalimbali za maisha. Anasema lazima ujue maisha ni ya kwako, na una haki ya kuchagua uishi namna gani, lakini anatoa ushauri kwamba ili ufikie mafanikio katika Nyanja yeyote lazima ujifunze kusema hapana kwa baadhi ya vitu, maana kila unaposema Hapana kwa jambo Fulani lisilo na umuhimu ujue unaacha nafasi ya Kusema ndiyo kwenye jambo la muhimu zaidi.

Karibu sana tujifunze mengine
1. Sema Hapana kwa shughuli nyingi zinazoweza kukuletea msongo wa mawazo na magonjwa ya moyo. Kujikita kwenye kazi nyingi mara kadhaa husababisha kujihisi umesongwa sana, huweza kupelekea kupatwa na msongo wa mawazo. Sema hapana kwa shughuli hizo. Na badala yake chagua shughuli chache tu ambazo ni za muhimu
2. Hutaweza kupata kipaji chako cha ubunifu kama utakua unasema ndio kwa kila mtu ambaye anaonekana anataka kufaidi kutoka kwako kimahusiano ambayo hayana mwelekeo, ama kwa watu wanaoku-control wewe, au kwa watu wanao kudanganya. Ukiwa na mazoea ya kusema ndiyo kwa hayo ujue hali yako sio nzuri.
3. Sema hapana kwa wivu. Kuna hali fulani ya kuwaonea wivu waliofanikiwa. Kuna wakati unaweza hata kuwasema vibaya kwa wengine. Wivu ni mwongozo wa kinachoendelea ndani yako. Badala ya kumuonea wivu mwenzako, furahia mafanikio yake, hii itakusaidia kua na hamasa ya kujifunza mbinu zilizompelekea akafika hapo. Ila ukiona wivu ina maana akili yako haitakua tayari kujifunza zile mbinu za huyo aliyefanikiwa hata kama unazifahamu.
4. Sema hapana kwa mahusiano ya kimapenzi yenye kuvuruga maisha yako. Usikubali kua mlevi (addict) wa mapenzi. Sio kila anayeonyesha kutaka kua na mahusiano na wewe, ni wa kumkubali tu. Kua na msimamo sema Hapana.
5. Unapokutana na mtu mwenye mawazo ambayo unayapinga vikali jaribu kufanya au kuzingatia yafuatayo:
· Usifanye mabishano naye, hana pointi ya maana na hutaweza kubadili akili zao
· Waache waelezee mawazo yao. Jaribu kujifunza kitu kutoka kwenye hayo mawazo. Pia jaribu kuheshimu mawazo yao.
· Tambua kila mtu anapenda kusikilizwa
· Sikiliza
6. Wewe ni wastani wa watu 5 unaotumia muda nao. Sema hapana kwa watu ambao hawana matokeo chanya kwako. Hao watu 5 hakikisha ni wale tu wenye kukusababishia wewe kusonga mbele, aidha kwa kukuhamasisha au kukupa changamoto zenye kuleta tija . Chagua marafiki kulingana na sifa ambazo zinafaa kukusongesha mbele kwenye ndoto au malengo yako.
7. Usifanye kitu chochote usichotaka kufanya. Hata kama umeambiwa kufanya usifanye. Maana utakapofanya utaishia kumchukia aliyekuamuru kufanya. Pia utakua unachukia shughuli hiyo unayoifanya bila kupenda kuifanya. Pia watu wengine hawatakua na imani na wewe tena. Usikubali kufanya hivyo.
8. Kulalamika ni kukimbiza fursa. Unapoacha kulalamika unaanza kuona kila hali ya fursa, unafungua mlango wa kupata mawazo mapya. When we stop complaining we are trusting that there is a better way and we are ready to hear it.
9. Sema hapana kwa watu wanaojaribu kukuweka chini na kukudharau. Lengo lao ni kuona upo chini yao au basi unalingana na nao. Sema hapana kwao, kwa kukaa mbali nao. Usiwape nafasi katika maisha yako, maana wakipata nafasi hata moja wataitumia kukuweka chini. Say no to people who aren’t right for you.
10. Sema hapana kwa social pressure. Unaweza kujikuta unafanya mambo kutokana na shinikizo la watu. Unaoa kwa sababu ya shinikizo, unakwenda kusoma kitu fulani kwa sababu ya shinikizo, unakwenda kuajiriwa mahali fulani kwa sababu ya shinikizo. Shinikizo zinaweza kuwa zinatoka kwa wazazi, marafiki au jamii kwa ujumla. Kumbuka utakapokutana na changamoto hutawaona hao waliokua wakikupa pressure ya kufanya hilo jambo.
11. Jifunze kujisamehe mwenyewe. Kabla ya kulala jaribu kukumbuka ni nani umekosana naye aidha yeye ndio mwenye kosa au wewe ndio mwenye kosa. Kuna hatua inafikia haijalishi ni nani yuko sahihi na nani amekosea. Wote ni kaka na dada na tupo hapa kwa muda mfupi tu. Hakuna haja ya kuwekeana vinyongo. Jifunze kusamehe, maana kwa kusamehe wengine unakua umejisamehe na wewe pia. Ni kupitia kujifunza kujisamehe mwenyewe kwanza ndipo utaweza kujifunza kuzungumza ukweli kwa wale wanaokuzunguka
12. Jifunze kusikiliza kwa moyo wa dhati. Unapokua na mazungumzo na watu utulivu ni mzuri. Sikiliza watu kwa umakini. Maana kila mtu anapenda kusikilizwa . Pia wakati wakuongea, jitahidi kuongea kwa step, usiongee kwa kasi. Maana kuongea kwa kasi kuna leta tafsiri ya uoga.
13. Sema hapana kwa maneno ya ziada na yasiyo na umuhimu. Kwa kawaida binadamu kwa siku anaongea maneno 2,500, jitahidi kupunguza angalau yafike hata 1,200 au chini ya hapo itakua ni nzuri zaidi. Jitahidi kua mtu wa kuhesabu maneno, sio kila unapojisikia kuongea tu basi unaongea.
14. Sema Hapana kwa makelele. Kelele zinaweza kua ni habari zenye hofu kutoka kwenye maredio au tv, makelele pia yanaweza kua ni umbea, mawazo hasi au ya hasira. Kaa mbali na makelele hayo. Kwanza anza kwa kutambua ni zipi kelele kwako. Kisha weka mpango wa kuepukana nazo. Mwanzoni inaweza isiwe rahisi lakini ukishazoea itakua rahisi. Maana kama umezoea kuangalia tv kila siku kuacha mwanzoni inakua tabu kidogo lazima uwe na nidhamu ya hali ya juu. Mimi mwenyewe ilikua ngumu kidogo lakini kwa vile nilikua na dhamira ya kweli, nimeshazoea kabisa, na sasa nakaribia mwaka sijaangalia tv kwangu.
15. Sema Hapana kwa uongo. Kuwa mkweli kwako binafsi kunapelekea mabadiliko yanayoonekana kwenye maisha yako. Uadilifu unaweza kubadili hata marafiki zako, familia yako, na hata kazi yako. Lakini si kila mtu anapenda kuona ukibadilika kwenye mwelekeo chanya. Kama watu 20,000 wanasema uongo, na mmoja pekee ndiyo anasema kweli, basi huyo mmoja yeye atawapita wengine wote kwa urefu. Kua mwadilifu tu ipo siku yako ya ng’ara. People will also come back for advice because you are a true souce of integrity.
16. Badili Mazungumzo. Unapogundua makelele yanayokuzunguka mara moja badili mazungumzo. Kama kuna habari mbaya kwenye tv zima tv, kama kuna watu uko nao wanaanza kupiga umbea, ondoka hapo au badilisha mazungumzo. Hata vitabu vya Mungu vinasema Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.
17. Ni rahisi sana kupokea habari hasi/mbaya ambazo kila mtu anajaribu kutulisha. Ndiyo maana habari zinazoshika nafasi kwenye vyombo vya habari ni zile habari mbaya/hasi, mfano habari za ajali, mapigano, mauaji n.k. Hata leo hii ukisikia mtu fulani amefanya kitu kizuri hiki na kile, wala hutataka hata kufuatilia, lakini upate taarifa kwamba kafanya tukio baya mfano kabaka, yaani utafutilia kila hatua, na utakua unamsimulia kila mtu. Hivyo ndivyo tulivyo binadamu. Usikubali kuingia kwenye mtego huu. Say no to it.
18. Sema Hapana kwa hasira za wakati uliopita. Pengine umekutana na jambo ambalo limekuudhi na ukakasirika sana, hasira inaendelea kukaa ndani yako, jitahidi kusema Hapana kwa hasira hizo. Unapokua na hasira hata uwezekano wa kutofanya vizuri ni mkubwa. Biblia inasema Hasira hukaa kifuani kwa mpumbavu. Usikubali kua mpumbavu.
19. Usiumize. Kama kitendo au jambo unalotaka kufanya unaona litaleta madhara kwa wengine basi acha usifanye. Mtu ambaye yuko katika hatari ya kuumizwa na wewe ni WEWE mwenyewe. Hivyo kwa kuacha vitendo vyenye kuwadhuru wengine, basi utakua pia umejisaidia usikumbwe na madhara.
20. Sema hapapana kwa vyakula vyenye kukusababishia kifo. Siku za leo kuna magonjwa mengi yanayosababishwa na vyakula tunavyokula mara kwa mara. Kwa vile madhara yake hatuyaoni hapo kwa papo, basi tunakua kama tumefungwa macho. Kisukari, presha au shinikizo la damu ni magonjwa ambayo haswa yanatokana na mwenendo wetu wa ulaji ambao sio sahihi Tambua ni vyakula au vinywaji gani ambavyo ni hatarishi. Sema hapana kwa vyote hivyo.
Asanteni sana
Tukutane wiki ijayo
Makala hii imeandikwa na Ndugu Daudi Mwakalinga mwandishi, mhamasishaji na mshauri katika masuala ya kilimo. Unaweza kuwasiliana naye kwa simu 0763 071007 au barua pepe
daudimwakalinga@yahoo.com au dd.mwakalinga@gmail.com

One thought on “Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu THE POWER OF NO.

Add yours

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: