Siku zote huwa nasema kwamba kuna ‘emergency’ chache sana kwenye
maisha. Ile hali kwamba jambo limetokea na watu wanashangaa limetokeaje ni
kuamua tu kutumia unafiki wetu wenyewe.
Ni sawa na shimo ambalo lipo njiani kwa muda mrefu lakini watu
wanaliangalia tu, siku moja linasababisha vifo watu wanasema ni ajali. Hapana
sio ajali, ni watu wamechagua kufa kwa njia hiyo. Kwa sababu shimo lilikuwa
linaonekana siku zote, lakini hakuna aliyejali.

Hivyo hivyo kwenye maisha yako, kuna vitu vingi sana ambavyo
unavipuuzia kwa sasa lakini kuna siku vitakukaba sana. Na wakati huo ndio
utaanza kuhangaika, utaanza kusumbua wengine kwamba kwa nini hawachukulii hali
yako kwa tahadhari. Bila ya wewe kujua na kukubali kwamba hakuna tahadhari kubwa
ila ni kitu ulichotengeneza wewe mwenyewe.

Kila siku inayoanza jiulize swali hili muhimu sana, je mambo
haya ninayofanya leo hayatengenezi tahadhari siku ya kesho? Au siku zijazo?
Mambo ninayoyapuuza leo hayajitengenezi na kuwa makubwa halafu siku moja
yakanizidi?

Ni kawaida ya binadamu kufanya vitu kwa mazoea ila mambo
yanapokuwa magumu tunasahau kwamba tumeyatengeneza wenyewe. Na kama wewe ni mtu
wa kulaumu utaanza kulaumu na uzuri ni kwamba hutakosa mtu wa kumlaumu.

Hakuna kitu kinachokea kwa ajali kwenye maisha yako, kila kitu
kinasababishwa na wewe mwenyewe ndiye unayesababisha. Kuwa makini na yale yote
unayofanya, yanaweza kukusababishia matatizo makubwa siku za mbeleni.

TAMKO LA LEO;

Najua chochote ninachofanya leo kina madhara kwenye maisha yangu
siku za baadae. Madhara haya yanaweza kuwa chanya au kuwa hasi. Nitahakikisha
maamuzi ninayofanya hayanipelekei kwenye madhara hasi ili niepuke kuwa na
dharura zisizo za msingi kwenye maisha yangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 196 kesho, Like page yangu ya
Coach
Makirita Amani
uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha
kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.

TUPO PAMOJA.