Umekuwa ukisikia mara nyingi kwamba kosa sio kutenda kosa, bali
kosa ni kurudia kosa. Hii ikiwa na maana kwamba unapofanya jambo kwa mara ya
kwanza na ukapata majibu ambayo hukutegemea kupata, tunaweza kukusamehe. Ila
tunatarajia kwamba uwe umejifunza kwamba njia uliyotumia mwanzo haileti majibu
unaotaka.

Sasa kama wewe utarudia tena kufanya vile vile na ukapata majibu
yale yale ambayo hukuyataka ndio tunasema kwamba wewe unafanya makosa. Nafikiri
tumeelewana vizuri hapo kwenye kosa, na unajua ni makosa gani ambayo umechagua
kuwa unayafanya tena na tena.

Sasa leo nataka nikuambie kitu kingine kizuri ambacho kinaweza
kuendana na hiko. Una sababu moja tu, nyingine zote ni kuchagua mwenyewe. Kwa
maana nyingine unaweza kuwa na kisingizio mara moja tu, baada ya hapo umeamua
mwenyewe na huna sababu au kisingizio chochote.

Kwa mfano; kwa nini kila siku unasema utaanza biashara ila
huanzi? Sababu ya kweli, sina mtaji. Swali hilo tena miaka mitano baadae, kwa
nini mpaka sasa hujaanza biashara… hapa ukisema tena huna mtaji sio sababu
tena, maana yake unajua kabisa kwamba huna mtaji na hufanyi jitihada zozote
kutafuta mtaji huo.

Usipende kutafuta sababu(visingizio), ila kama haikwepeki, basi
sababu iwe mara moja tu. Kama utaendelea kutuambia sababu ile kila siku sio
sababu tena bali umeamua kuishi maisha hayo. Hivyo tafadhali sana, usitupigie
tena kelele, tumeshasikia sababu yako na umeshatuambia kwamba umekubali kuishi
nayo.

TAMKO LA LEO;

Najua nina nafasi moja tu ya kuwa na sababu au kisingizio. Ila
baada ya hapo siwezi tena kutumia kisingizio hiko kwa sababu nitakuwa nimeamua
mwenyewe. Kuanzia leo nitakwepa kutoa sababu na kama sababu haikwepeki nitatoa
mara moja tu.

Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita
Amani
uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi
yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.

TUPO PAMOJA.