Habari za leo mpenzi msomaji wa blog mbalimbali zinazoendeshwa
na AMKA
CONSULTANTS. Naamini unaendelea vizuri na harakati zako za kuboresha maisha
yako. Na pia naamini TUPO PAMOJA ukiendelea kujifunza na kuhamasika kupitia
makala mbalimbali zinazopatikana kwenye blog zako zinazoendeshwa na AMKA
CONSULTANTS.
Kama unavyojua lengo kubwa la AMKA CONSULTANTS ni kukuwezesha
wewe kuishi maisha bora sawa sawa na uwezo wako. Hapo ulipo una uwezo mkubwa
sana wa kufanya mambo makubwa zaidi ya unavyofanya sasa. Ila mfumo wa elimu
uliopitia na malezi uliyokulia vimekufanya ushindwe kufikia uwezo wako
mkubwa.
Kama umekuwa unafuatilia blog zetu mbali mbali na ukawa
unafanyia kazi yale ambayo umekuwa unajifunza, utakubaliana nami kwamba maisha
yako umeona yanabadilika, hata kama ni kwa kiasi kidogo. Kama hiki ndio
kinachotokea kwenye maisha yako basi nakusihi endelea kufanyia kazi na utazidi
kuona mabadiliko makubwa zaidi.
AMKA CONSULTANTS ilianza na blog ya AMKA MTANZANIA na baadae
zilianzishwa blog nyingine kutokana na mahitaji tofauti ya wasomaji wetu. Blog
hizo ni KISIMA CHA MAARIFA, ambayo
unalipia kuwa mwanachama, MAKIRITA AMANI na JIONGEZE
UFAHAMU.
Kupitia blog hizi umekuwa unajifunza mambo mengi na mazuri sana.
Kwa sababu makala zinazowekwa kwenye blog hizi zinatofautiana na zinalenga
maeneo tofauti tofauti ya maisha yako ikiwemo kazi, biashara na hata maisha kwa
ujumla.
Napenda kuchukua nafasi hii kuwajulisha wasomaji wote kwamba
kutakuwa na mabadiliko kwenye blog hizi zinazoendeshwa na AMKA CONSULTSNTS.
Makala ambazo zilikuwa zinawekwa kwenye JIONGEZE UFAHAMU sasa zitahamishiwa
kwenye AMKA MTANZANIA na makala zilizokuwa zinawekwa kwenye MAKIRITA AMANI sasa
zitahamishiwa kwenye KISIMA CHA
MAARIFA. Na blog hizi mbili, MAKIRITA AMANI na JIONGEZE UFAHAMU
zitafutwa.
Kwa nini mabadiliko haya?
Kama umekuwa msomaji mzuri wa blog hizi utakuwa uliona tatizo
ambalo lilijitokeza kama mwezi mmoja uliopita. Wasomaji ambao walikuwa wanapokea
makala za blog moja wapo kwa email ghafla waliacha kupata makala. Wakati huo
makala zilikuwa zinatumwa kama kawaida. Kutokana na tatizo hili ilibidi kutafuta
suluhisho la haraka ili wasomaji waendelee kupata makala zetu nzuri. Tulipata
suluhisho la muda lakini halitadumu kwa muda mrefu, siku zio nyingi tutaingia
tena kwenye tatizo kama lile. Na hii inatokana na sababu ya pili ya kuondoka
kwenye blog hizi ambayo ni kuwa zimekuwa zinaendeshwa bure.
Blog inapokuwa imehifadhiwa bure na kutumia jina la bure, kuna
baadhi ya vitu huwezi kuvibadili. Sasa hili linakwenda tofauti na kile ambacho
nataka wewe msomaji ukipate. Kuna wakati nataka kufanya kitu ambacho ni cha
tofauti lakini nashindwa kwa sababu blog imehifadhiwa bure na hivyo huwezi
kubadili baadhi ya vitu.
Sababu nyingine ni kwamba nina sehemu kubwa ya kuhifadhi blog
hizi ambayo ninailipia kila mwaka ambayo kwa sasa imehifadhi KISIMA CHA MAARIFA,
sasa ni vyema kutumia sehemu hii ambayo tunailipia gharama kubwa kuweka mafunzo
ambayo yataendelea kuboresha maisha yako.
Na sababu ya mwisho tunayoweza kujadili hapa ambayo imepelekea
kufanya mabadiliko haya ni wewe msomaji uweze kupata makala zote nzuri kwenye
blog chache. Ni kweli kuna umuhimu wa kutenganisha mambo lakini ni vyema wewe
kama msomaji ukijua unapata makala zako zote nzuri kwenye sehemu chache ambazo
unaweza kuzitembelea kila siku na kutumia muda wao vizuri.
KISIMA CHA MAARIFA ni kulipia, je sisi tuliokuwa
tunapata makala bure ndio mwisho?
Ni kweli kabisa ili uweze kusoma makala kwenye KISIMA CHA MAARIFA inabidi uwe umejiunga
na ulipie. Ila kwa sasa kwa kipengele hiki cha KURASA 365 ZA MWAKA 2015 wasomaji
wote wataendelea kuzipata hata kama hawajajiunga na kulipia. Ila nakusihi sana
kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA ufanye hivyo mara moja kwani unakosa
mengi na utaendelea kukosa mengi. Bonyeza maandishi haya KUJIUNGA
NA KISIMA CHA MAARIFA. Kuendelea kupata makala za KURASA 365 hakikisha
unatembelea KISIMA CHA MAARIFA kila
siku, na pia jiunge kwa kuweka email yako unapokuw akwneye KISIMA na utatarifiwa
kila makala inapokwenda hewani.
Asante sana kwa kuendelea kujifunza na kufanyia kazi yale ambayo
yanawekwa kwenye mitandao hii. Tunaendelea kukuahidi kwamba tutakuletea makala
bora kabisa zitakazo boresha na kubadili maisha yako.
TUPO PAMOJA.
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz