Habari za leo mpenzi msomaji wa KISIMA CHA MAARIFA.

Naamini kwmaba unaendelea vizuri na unaendelea kujifunza na kuhamasika na pia kuchukua hatua ya kuboresha maisha yako.

Hili ndio lengo kuu la mitandao hii kuhakikisha maisha yako ya leo ni bora kuliko yalivyokuwa jana.

Kama nilivyosema kwenye tangazo la awali, kumekuwa na mabadiliko yanayoendelea kwenye blog hizi. Hii yote ni kukuletea wewe huduma bora ambazo zitakuwezesha kuwa bora zaidi.

Katika muendelezo huu wa mabadiliko, leo kuna makala nyingi zilikuwa zinahamishwa na hivyo kama umekuwa mpokeaji wa makala hizi kwa njia ya email utakuw aumepata email nyingi sana kw awakati mmoja. Utakuw aumepata email zaidi ya 600 kwa wakati mmoja. Hizi ni email nyingi sana na zimeleta usumbufu mkubwa kwako.

Mimi pia nimepata email hizo nyingi kwenye email ninayoitumia kama msomaji wa kawaida. Zimekuwa usumbufu mkubwa kwangu na imenichukua muda kuzifuta ili niweze kubaki na email muhimu ninazotakiw akujibu.

Naomba kuchukua nafasi hii kukuomba radhi kwa tatizo hilo, na ningekuomba uchukue muda kidogo na uzifute email hizo zote. huna haja ya kuzisoma zote wka sababu kama umekuwa msomaji kwa kipindi kirefu basi makala hizo zote ulishazisoma.

Asante sana kwa kuendela kuw apamoja katika safari hii ya kuboresha maisha yetu kila siku.

Naamini tutaendele akuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha yako.

Karibu sana.

Kama hukuyasoma maelezo ya mabadiliko tafadhali YASOME HAPA.

Pia kuna badiliko moja ambalo halikuelezwa hapo. SASA MAKALA ZA BIASHARA LEO ZITAPATIKANA KWA WALIOJIUNGA NA MAKALA ZA KURASA 365 ZITAPATIKANA BURE KWA WOTE.

Pia kama bado hupati makala za mtandao huu kwa njia ya email, unapokuwa unasoma makala, angalia upande wa kulia kama unatumia kompyuta au shuka chini kama unatumia simu na utakuta sehemu imeandikwa WEKA EMAIL YAKO KUPATA MAKALA na uweke email yako hapo, dhibitisha na kisha utakuw aunapewa taarifa za makala kila zinapowekwa.

TUPO PAMOJA.