Sababu namba moja kwa nini watu wengi hawafanikiwi! Hawapo tayari.

Je wewe upo tayari?

upo tayari

Je upo tayari kufanya tofauti na wafanyakazi wenzako wote wanavyofanya kazi zao?

Je upo tayari kuendesha biashara yako kwa utofauti na vile wafanyabiashara wengine wanavyoendesha?

Je upo tayari kwenda hatua ya ziada na kumridhisha mteja wako, hata kama utaingia hasara?

Je upo tayari kuacha kushabikia habari ambazo hazina msaada wowote kwako?

Je upo tayari kuacha kupoteza muda wako kuangalia tv, au kufuatilia maisha ya watu ambao hawajui hata kama wewe upo?

Je upo tayari kuacha kufanya mambo ili uonekane na badala yake kufanya mambo yatakayoleta mabadiliko?

Je upo tayari kuamka asubuhi na mapema wakati wengine wamelala na wewe ukatumia muda huu kusonga mbele zaidi?

SOMA; njia rahisi ya kufikia uhuru wa kifedha.

Je upo tayari kutatua matatizo ya watu yanayohusiana na kile unachofanya, hata kama hawakulipi kwa sasa?

Je upo tayari kuwasikia watu wanakuambia huwezi, utashindwa, unapoteza muda wako, na bado ukaendelea kufanya?

Je upo tayari kuchekwa na kuonekana wewe umeshindwa ka kile ulichojaribu kufanya na bado ukarudia kukifanya tena, na wakati huu ukiwa makini zaidi?

Je upo tayari kusimamia kile unachoamini, kutekeleza kile unachoahidi?

Je upo tayari kutokuenda viwanja wakati wenzako wote wanakwenda viwanja, na wewe kutumia muda huo kufanya miradi yako itakayokuletea mafanikio?

Je upo tayari kuacha kulalamika na kulaumu serikali, ndugu zako, wazazi wako, mwenza wako, hali ya hewa, hali ya uchumi na kila kitu kwamba ndio kinakufanya wewe kuwa na maisha magumu?

Je upo tayari kuamini kwamba wewe una uwezo mkubwa na kwamba hufanani na mtu mwingine yeyote na hivyo hukubali kulinganishwa na mwingine?

Je upo tayari??

Mara ya mwisho wakati naangalia kama hupo tayari kwa mambo hayo na mengine mengi yanayofanana na hayo(kama upo tayari unayajua) basi ni vigumu sana kufikia mafanikio?

Lakini habari njema ni kwamba bado una muda wa kutosha wa kujiweka tayari na baadae kufaidi matunda mazuri ya wewe kuwa tayari.

Kama upo tayari hongera sana na tuendelee na safari yetu ya mafanikio. Kama bado haupo tayari niandikie kwenye makirita@kisimachamaarifa.co.tz niambie ni nini kinakufanya usiwe tayari.

Hatutaki kumuacha hata mmoja nyuma, miaka kumi ijayo kila mmoja wetu atakuwa mbali sana. Ila kama wewe utaamua kubaki nyuma peke yako hakuna wa kukuzuia.

TAMKO LA LEO;

Hivi kweli mimi nipo tayari kwa suluba zote nitakazokutana nazo kufikia mafanikio makubwa. Nipo tayari kwa yote yatakayonitokea kwenye safari hii niliyochagua? Naamini nipo tayari. Na ninatangaza leo kwamba hakuna wa kunirudisha nyuma, ni mpaka nifike pale ninapotaka kwenda au nifie njiani, hakuna kurudi nyuma. Nimeamua leo na nitaendelea kuweka juhudi, maarifa, kujituma na uvumilivu mpaka nipate kile ninachokitaka.

Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.