Kuna watu huwa wanasema eti maisha hayana fomula. Napenda sana ninapokutana na watu hawa, maana huwa nawauliza wanaelewaje hiyo kauli kwamba maisha hayana fomula? Nilichokuja kugundua wengi wanasema huo msemo kwa sababu wamesikia wengine wanasema. Na wengi pia wanafikiria kwamba maana ya kwamba maisha hayana fomula ni mtu anaweza kufanya kitu fulani kwa njia fulani na wewe ukafanya kitu hiko hiko kwa njia hiyo hiyo na usipate majibu aliyopata mwingine.

Sasa kama na wewe unafikiri kwa dhana hiyo ndio maisha hayana fomula, basi unapotoka kwa sababu kuwepo kwa hali hiyo ndio kunadhibitisha vizuri kwamba maisha yana fomula.
Ila kitu kimoja unachotakiwa kukijua ni kwamba fomula ya maisha ni tofauti kwa kila mtu. Hivyo ili uweze kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako, ni lazima kwanza uijue fomula yako halafu ndio uende nayo kila siku. Kama utatumia fomula za wengine utaishia kupata majibu ya kawaida na wakati mwingine utashindwa kabisa.
Maisha yana fomula, ila kwa kuwa kila mmoja ni tofauti, hivyo hivyo kila mmoja ana fomula yake. Kuna fomula ambazo ni sawa kwa wote, hizi ni zile za kuishi maisha ya kawaida. Ila kufikia mafanikio makubwa ni lazima ujitengenezee fomula yako mwenyewe.
Na mara nyingi ukifanya yale ambayo watu waliofanikiwa wanafanya, na wewe ukaongeza ubunifu na uwezo wako wa ziada ndio fomula yenyewe. Na wala huhitaji elimu kubwa kuweza kuing’amua fomula yako ya mafanikio.
Maisha yana fomula na kila mmoja ana fomula yake maalumu. Ijue yako na itumie.
TAMKO LA LEO;
Maisha yana fomula, na kila mmoja wetu anaweza kuwa na fomula yake tofauti. Nitaijua fomula yangu kwa kuanza kufanya yale ambayo watu waliofanikiwa wanafanya na nitaongeza ubunifu na kuweka uwezo wangu wa kipekee. Najua kwa njia hii hakuna kitakachonizuia kufikia mafanikio makubwa.
Tukutane kwenye ukurasa wa 207 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.