Wote tunajua kwamba maisha yako ni wastani wa watu watano wanaokuzunguka.
Kama watu watano wanaokuzunguka wanakukatisha tamaa na kukutudisha nyuma huwezi kufanikiwa hata ukiwa na juhudi kiasi gani.
Kama watu watano wanaokuzunguka wanakupa moyo na kukusaidia ni lazima utafanikiwa.
Fanya hilo zoezi hapo juu na hakikisha unawakata watu watano leo na unakuja na tano bora yako kwa ajili ya mafanikio yako.
Ukishaipanga tano bora yako, anza kutengeneza mazingira mazuri ya kuwa karibu zaidi na hao watano ili unufaike zaidi.
Wasiliana nao kwa siku au ujumbe au ana kwa ana. Jua ni vitu gani wanafanya na kama unaweza kusaidia. Waambie kile unachofanya na omba ushauri wao pia.
Utashangaa njia yako ya mafanikio itakuwa rahisi na yenye furaha.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani.
#UJUMBE_LEO; Watu Watano Wa kuambatana nao Na Watu Watano Wa Kuwakimbia Haraka.
