Mpaka sasa unajua kwamba mafanikio hayatokei mara moja kama ajali. Yaani sio kwamba siku moja utaamka na ukute mafanikio hayo yamekuja mara moja. Bali maisha unayoishi kila siku ndio yanayotengeneza mafanikio yako. Mafanikio ni maamuzi madogo madogo unayofanya kila siku.

KILA SIKU NI KAMA UPO NJIA PANDA, JE UNACHAGUA NJIA IPI? KAZI NI KWAKO.
KILA SIKU NI KAMA UPO NJIA PANDA, JE UNACHAGUA NJIA IPI? KAZI NI KWAKO.

Sasa kushindwa nako ni hivyo hivyo, hutaamka siku moja na kukuta ndio umeshindwa, bali kushindwa ni maisha ambayo unayachagua kila siku. Kuna tabia zako za maisha ya kila siku ambazo zikikusanyika ndio zinakuletea maisha ya kushindwa.

Kwa mfano kama una matumizi mabovu ya fedha, matumizi yako yanazidi kipato chako na sio matumizi ya msingi. Hutajikuta umeshindwa mara moja. Kidogo kidogo kila siku utaendelea kupoteza fedha, utaendelea kukopa sehemu mbali mbali, hii ni tabia unayofanya kila siku halafu siku moja unagundua kwamba huna akiba yoyote na una madeni makubwa sana.

Labda kushindwa kwako kunatokana na afya mbaya, hii nayo haitokei mara moja. Ni tabia zako za kila siku ndio zinatengeneza afya yako. Unakula nini, unafanyaje mazoezi unaipa afya yako kipaumbele gani.

Kama ukiwa makini na maisha yako, utaona mapema kabisa kama kweli unaelekea kushinda au kushindwa. Japo ni kitu ambacho kipo wazi, bado wengi hujifanya hawalioni hili na kuanza kutafuta sababu za nje kwa nini wameshindwa. Ukitaka sababu utazipata nyingi sana, ila sababu ya kweli unaikwepa ambayo ni maisha uliyochagua kuishi.

Chagua leo maisha ya mafanikio, kila kitu unachofanya jiulize je kinakupeleka kwenye kushinda au kushindwa. Kama ni kushindwa achana nacho mara moja. Usiendelee kupoteza muda wako.

TAMKO LA LEO;

Najua kwamba kushindwa hakutokei mara moja bali na tabia ambayo mtu unaipalilia kila siku. Kuanzia sasa nitakuwa makini na mambo ninayofanya kila siku. Nitajiuliza kabla ya kuendelea, je jambo hili ninalofanya linanipeleka kwenye mafanikio au kushindwa. Kama linanipeleka kwenye kushindwa, nitaliacha mara moja.

Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.