Mara nyingi nikiwa nafanya kazi ambayo haihitaji umakini sana na eneo likawa na kelele zozote ndogo ndogo zinazoweza kunihamisha mawazo, huwa navaa spika za masikioni na kusikiliza muziki kwa sauti ya chini. Hii ni njia moja ambayo imekuwa ikinisaidia sana kuweza kufanya kazi hata kama eneo lina kelele. Na muziki ninaosikiliza huwa ni nyimbo ambazo nimewahi kuzipenda sana zamani.

Jana nilikuwa nasikiliza nyimbo hizi wakati nafanya kazi, na ukawa unapigwa wimbo mmoja wa FM Academia unaitwa heshima kwa wanawake. Huwa sijui maneno mengi kwenye wimbo huo ila napenda mpangilio wa muziki. Sasa jana nilisikia kauli moja kwenye wimbo huo ambayo sikuwahi kuisikia mara zote ambazo nimekuwa nasikia wimbo huo. Kauli hiyo ilikuwa kwamba DUNIA NZIMA ITAMPISHA MTU AMBAYE ANAJUA NI NINI ANATAKA.

JE UNAJUA NI NINI HASA UNACHOTAKA KWENYE MAISHA YAKO?
JE UNAJUA NI NINI HASA UNACHOTAKA KWENYE MAISHA YAKO?

Nakubaliana na kauli hiyo kwa asilimia 100 ya kwamba kama unajua ni nini unataka, basi dunia nzima itakupisha ili upate hiko unachotaka. Hakuna mtu au kitu chochote ambacho kinaweza kukuzuia wewe kupata kile ambacho kweli umedhamiria kukipata.

SOMA; Kufanikiwa, Jua Kitu Ambacho Wengine Hawajui, Ila Usiwe Mchoyo.

Sasa kama hiyo ni kweli, mbona watu wengi wanataka vitu lakini hawavipati? Jibu ni kwamba wengi wanataka vitu, ila hawajajitoa kweli kuvipata. Ndio maana wanajaribu na wakishindwa mara moja tu wanakimbia na kusema haiwezekani. Ila wale wanaojua ni nini hasa wanachotaka, na wakajitoa kweli, hata wakishindwa wanajua sio mwisho bali ni sehemu tu ya safari. Wanaendelea kung’ang’ana mpaka wapate kile wanachokitaka. Na sheria ya maisha ni kwamba kama utakuwa king’ang’anizi, basi hakuna atakayeweza kuvumilia usumbufu wako, utapewa tu kile ambacho unataka.

Je unajua ni nini hasa unachotaka kwenye maisha yako? Je umejitoa kweli kuhakikisha unapata kitu hiko? Kama jibu ni ndio, hongera sana maana una uhakika wa kukipata. Kama jibu ni hapana, pole kwa sababu unaendelea kupoteza muda wako.

TAMKO LA LEO;

Nimejua ya kwamba dunia nzima itanipisha kama kweli nitakuwa najua ni nini ninachotaka na nikajitoa kweli ili kuweza kukipata. Nimejitoa sasa na nitaweka juhudi na maarifa mpaka pale nitakapopata vitu hivi vitatu(vitaje); 1._____ 2. ______ 3. _______. Najua hakuna kinachoweza kunirudisha nyuma kwenye maamuzi yangu haya makubwa na muhimu.

Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.