KITABU CHA SEPTEMBA; Guide To Investing(Muongozo Wa Uwekezaji).

Hongera kwa kuendelea kuwa msomaji na mfuatiliaji mzuri wa AMKA MTANZANIA. Naamini kupitia mtandao huu umekuwa ukipata maarifa na hamasa ambazo zimewezesha maisha yako kuwa tofauti na yalivyokuwa hapo awali. Hongera sana kwa hilo.
Kila mwezi, umekuwa unapata kitabu kimoja kizuri sana cha kujisomea. Kwa kusoma vitabu hivi vinavyotolewa kila mwezi unapata maarifa ambayo yanayafanya maisha yako kuwa bora zaidi ya yalivyokuwa hapo awali. Mpaka sasa umeshapata vitabu vingi sana kwenye mpango huu, kikubwa ni wewe kufanyia kazi yale ambayo unajifunza.
Mwezi huu wa septemba unapata nafasi ya kupokea kitabu kingine kizuri sana kutoka AMKA MTANZANIA. Na kitabu cha mwezi huu kinaitwa RICH DAD’S GUIDE TO INVESTING ambacho kimeandikwa na mwandishi Robert Kiyosaki, mwandishi maarufu wa kitabu RICH DAD POOR DAD.

 
Robert Kiyosaki ameandika vitabu vingi sana kuhusu fedha na uwekezaji. Na kitabu chake cha kwanza, RICH DAD POOR DAD, kinatoa mwanga sana kuhusu mambo ya fedha na utajiri. Nimekuwa nasisitiza sana watu wasome kitabu hiko, na kama bado hujakipata na kusoma, jiunge na AMKA MTANZANIA kwa kuweka email yako kisha utapata kitabu hiko.
Katika kitabu cha mwezi huu, GUIDE TO INVESTING utajifunza kila kitu ambacho unataka kukijua kuhusu uwekezaji. Robert ameuvunja uwekezaji kwenye vipande vidogo vidogo sana ambapo hata mtoto mdogo anaweza kuelewa.
 
Kila mtu anatakiwa kuwa mwekezaji, ndio nimesema kila mtu. Hivyo kama mpaka sasa hujaanza kuwekeza, umeshaanza kubaki nyuma, ila kama utaanza sasa, utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kufikia uhuru wa kifedha.
Watu wengi hawana elimu ya uwekezaji. Kuna uwezekano mkubwa hujui hisa ni nini au kama unajua ni nini ukawa hujui wewe utafaidikaje kwa kununua hisa. Kupitia kitabu hiki utaelewa vizuri sana hisa ni nini, unafaidikaje kwa kununua hisa, ni wakati gani mzuri wa kununua na hata wa kuuza.
 
Kwa wale ambao wanajua kidogo kuhusu uwekezaji wamekuwa wakisema uwekezaji ni hatari sana(risk), sasa Robert kiyosaki anakuambia sio kwamba uwekezaji ndio hatari, bali mwekezaji ndio hatari. Watu wengi ambao wanapata hasara kwenye uwekezaji ni wale ambao hawana elimu nzuri ya uwekezaji. Kwa kusoma kitabu hiki utapata elimu nzuri ya uwekezaji ambayo itakuondoa kwenye kundi la kupata hasara.
Unapoamua kuwa mwekezaji usikubali kabisa kuwa wa kawaida tu. Wawekezaji wa kawaida ndio ambao wamekuwa wanapata hasara kubwa. Kuna sheria moja unasema kwamba asilimia 10 ya watu wote duniani, wanamiliki asilimia 90 ya utajiri wote wa dunia. Na asilimia 90 ya watu wote duniani, wanamiliki asilimia 10 ya utajiri wote wa dunia. Yaani kuna watu wachache sana wanaomiliki utajiri mkubwa sana, na kuna watu wengi wana wanaomiliki utajiri mdogo.
 
Hawa wachache wanaomiliki utajiri mkubwa ni wale waliokataa kuwa wa kawaida, na kutaka kupiga hatua ya ziada kwenda mbele zaidi. Hawa wengi ambao wana utajiri kidogo ni wale ambao wameamua kuwa wa kawaida.
Kuna mambo mengi sana ya kujifunza kwenye kitabu hiki, hapa najaribu kukudokezea tu, ili unapoanza kusoma ujue ni nini unakwenda kupata kwenye kitabu hiki.
Kwa mfano kuna vitu vitatu muhimu sana kwa mwekezaji kuwa navyo ili aweze kufanikiwa kwenye uwekezaji. Cha kwanza ni elimu, unahitaji elimu ya uwekezaji, kama ambavyo utaipata kwenye kitabu hiki. Cha pili ni uzoefu, hataukiwa na elimu kubwa kiasi gani, bado unahitaji uzoefu halisi. Na cha tatu ni fedha za ziada, unahitaji fedha ambazo huna presha nazo ndio uziwekeze, maana hapa hutasukumwa kuuza ili upate fedha.
Nachokusihi sana wewe msomaji ni kusoma kitabu hiki, kitakupa maarifa mengi sana akuhusu uwekezaji na hata kuhusu biashara kwa ujumla. Kwa sababu uwekezaji ni biashara na hivyo misingi yote ya biashara utajifunza kwenye kitabu hiki.
 
Kitabu hiki kina masomo 16 muhimu ya uwekezaji, kina aina za uwekezaji na aina ipi ni nzuri ili uweze kufikia mafanikio makubwa. Pia kupitia kitabu hiki utajifunza jinsi tabia za watu zinavyoingilia mafanikio yao kupitia uwekezaji.
Kama unaishi na kama siku moja ungetaka kuwa na uhuru wa kifedha, soma kitabu hiki. Na kama utaacha kukisoma, kwa sababu umechagua kutokufanya hivyo, usije ukalaumu watu utakapofikia wakati ambapo huwezi tena kufanya kazi na wakati huo pia huna kipato cha uhakika. Ukianza kuwekeza leo, miaka kumi ijayo utakuwa mbali sana katika swala la kifedha.
Kupata kitabu hiki bonyeza maandishi haya kama umeshajiunga na AMKA MTANZANIA, na kama bado hujajiunga bonyeza maandishi haya na uweke taarifa zako kisha utatumiwa kitabu kwenye email.
Hiki ni kitabu kizuri sanaa ambacho hutakiwi kukosa kukisoma kwenye maisha yako, kipate leo na anza kukisoma.
Soma kitabu hiko na ukikimaliza na ukawa unahitaji ushauri zaidi kuhusu uwekezaji hasa kwa hapa kwetu Tanzania, tuwasiliane. Tafadhali nitafute ukiwa umeshamaliza kusoma kitabu hiko na nitakushauri vizuri zaidi kuhusu uwekezaji kwa hapa kwetu.
Nakutakia kila la kheri katika kujifunza kuhusu uwekezaji. Endelea kuongeza maarifa, ni muhimu sana kwa mafanikio yako.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani.
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: