Kila mmoja wetu anapenda kufanikiwa kwenye maisha, na ndio kitu ambacho tumekuwa tunafanyia kazi kila siku.

Lakini wakati tunakazana kufikia mafanikio makubwa, kuna sumu zinazotunyemelea ambazo zinatuzuia kufikia mafanikio makubwa.

Kuna sumu nyingi za mafanikio, ila kati ya hizo kuna sumu kubwa mbili ambazo zikishakuingia, wewe mwenyewe ndio unaua safari yako ya mafanikio.

FANYA KAZI YAKO, USIYUMBISHWE NA KILE WENGINE WANASEMA.
FANYA KAZI YAKO, USIYUMBISHWE NA KILE WENGINE WANASEMA.

Sumu ya kwanza ni kukosolewa. Utakapoanza kufanya kitu cha tofauti kuna watu wataanza kukukosoa. Wengine watajiona mafunzo kuliko wewe, watakuambia unakosea, watakuambia huwezi, watakuambia utashindwa na maneno mengine mengi. Hii ni sumu kubwa sana iliyowazuia wengi, huenda hata wewe mwenyewe kuweza kufikia mafanikio makubwa.

Epuka sana sumu hii, mtu yeyote anapokukosoa kwa kukukatisha tamaa, usimsikilize, wewe kazana kuboresha. Usisikilize neno la mtu mwingine yeyote, hakuna anayejua zaidi yako kwa kile unachofanya na uwezo ulionao.

SOMA; Usiwasikilize Watu Hawa.

Sumu ya pili ni sifa. Utakapoanza kufanya vizuri kuna watu watakusifia. Watu watakuambia unafanya vizuri, watakuambia unaweza sana na maneno mengine mazuri ya sifa. Lakini wewe usilewe maneno haya na kuanza kujiona wewe ndio kila kitu. Bado una kazi kubwa sana ya kufanya, hiko ulichopata ni kipande tu, kuna mengi unahitaji kuyafanyia kazi.

Epuka sumu hii kwa kushukuru pale unaposifiwa, lakini sahau sifa hizo mara moja na rudi kufanya kazi. Usikubali sifa hizo zikupe kiburi kwa sababu zitakuondoa kwenye njia nzuri ya kufikia mafanikio makubwa zaidi.

TAMKO LA LEO;

Nimejua kuna sumu mbili kubwa sana ambazo zinanizuia kufikia mafanikio. Sumu hizi ni kukosolewa na kusifiwa. Kuanzia sasa sitakubali sumu hizi ziwe kikwazo kwangu. Nitaendelea kuweka juhudi na kuboresha bila ya kujali watu wanasema nini. Kwa sababu najua kwa vyovyote vile, nina nafasi kubwa ya kuboresha hiki ninachofanya.

Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.