Ili watu wakuheshimu ni lazima wewe mwenyewe kwanza ujiheshimu.
Ili ufikie mafanikio makubwa kwenye maisha yako ni lazima ujiheshimu.

Lakini watu wengi wamekuwa hawajiheshimu, na hii imekuwa inawazuia kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yao.
Na kujiheshimu ninakozungumzia hapa hakuishii tu wewe kuwa mtu mwema na kuwa na maadili mazuri. Bali kunakwenda mbali zaidi mpaka kwenye mambo yako mengine binafsi.
Je unatekeleza mipango uliyojipangia? Kama umepanga kitu wewe mwenyewe, halafu unaacha kukitekeleza, kweli utasema unajiheshimu?
Kama muda ni wako mwenyewe, na unajua ni wa thamani, lakini bado unaupoteza, kweli unajiheshimu?
SOMA; Unahitaji Mipango Mingapi Ili Kutangaza Kushindwa?
Kama unajua uwezo wako ni mkubwa na unaweza kufanya zaidi ya unavyofanya sasa, lakini unaamua kufanya tu kawaida, kweli unajiheshimu?
Tafadhali sana, anza kufanya kile ambacho umepanga kufanya, anza kuongeza ubora ambao upo ndani yako, na utazidi kujiheshimu na wengine watakuheshimu zaidi.
Kuna watu huwa wanalalamika kwamba watu wenye hela wanaheshimika kuliko ambao hawana fedha. Pamoja na sababu nyingine nyingi, moja wapo ni kujiheshimu. Kuwa na fedha nyingi ni kielelezo kizuri cha kujiheshimu. Hakuna mtu ambaye hajiheshimu, haheshimu mipango yake, haendi hatua ya ziada anayeweza kufikia utajiri.
Jiheshimu zaidi na utapata mafanikio makubwa sana.
TAMKO LA LEO;
Najua nahitaji kujiheshimu zaidi ili niweze kufikia mafanikio makubwa. Najua kujiheshimu hakuishii tu kuwa mtu mwema na kuheshimu wengine, bali kunaanzia ndani yangu mwenyewe kwa kuheshimu mipango yangu, kwa kuheshimu uwezo wangu na kwenda hatua ya ziada. Nitazidi kujiheshimu kila siku ili niweze kufikia mafanikio makubwa.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.