Habari mwanafalsafa?
Ndio, wewe ni mwanafalsafa, na wala huhitaji kusubiri mpaka mtu akuite hivyo.
Chimbuko la neno falsafa au kwa kiingereza philosophy ni neno la kigiriki filosofia ambalo maana yake ni kupenda busara/hekima. Kwa kifupi ni kupenda kujifunza na kufikiri zaidi juu ya kile kitu unachofanya au vile unavyoishi.
Kwa kuwa lengo letu hapa ni kujifunza namna ya kuishi maisha mazuri kwetu na kwa wanaotuzunguka, yatakayotuletea furaha na mafanikio makubwa, basi sisi wote ni wanafalsafa wa maisha.
Leo katika mfululizo huu wa makala za falsafa mpya ya maisha, ninakushirikisha fursa kubwa na nzuri sana ya kuweza kuimarisha falsafa ambayo unajijengea na unaendelea kujijengea kwenye maisha yako.
Kama tunavyojua kitu chochote inahitaji kutunzwa sana, la sivyo mazingira magumu yanakimaliza. Chukua mfano wa mtoto mchanga, kama asipotunzwa vizuri, mazingira yanayomzunguka ni hatari sana kwake. Baridi ambayo wewe mtu mzima unaweza kuivumilia, inaweza kumuua mtoto mchanga aliyezaliwa leo. Hivyo matunzo ni muhimu sana, hasa wakati wa uchanga.
Hivi ndivyo ilivyo pia kwa kitu chochote kipya unachojifunza, mwanzoni unakuwa mchanga na unakuwa na hatari kubwa sana ya kukianza. Labda umejifunza kuhusu kuongeza tija kwenye kazi yako na unaamua sasa kwamba utaweka juhudi kubwa kwenye kazi na kuongeza thamani. Unafika eneo lako la kazi na kuanza kutekeleza hayo na nini kinatokea? Kila mtu anaanza kukuona wewe ni wa ajabu, ya nini unajihangaisha, fanya kawaida, hakuna anayekulipa zaidi na maneno mengi ya kukukatisha tamaa. Na nini kinatokea? Ile mbegu ya ubora uliyopanda inakufa na unarudi kuwa kawaida.
Najua hali hii imeshakutokea mara nyingi na kwenye maeneo mbalimbali.
Sasa usikubali hili likutokee kwenye falsafa hii mpya ya maisha unayojijengea. Na ili kuzuia hilo lisitokee kuna SEMINA nzuri sana itakayoendeshwa kwa njia ya mtandao inayokwenda kwa jina MIMI NI MSHINDI. Hii ni semina ambayo itakujengea fikra sahihi na kukupa mbinu za kuweza kufikia ushindi kwenye jambo lolote unalofanya na maisha kwa ujumla.
Na lengo la FALSAFA MPYA YA MAISHA ni nini? Kukujengea wewe uwezo wa kuishi maisha ya ushindi. Kwa sababu huu basi, usiache kujiunga na semina hii nzuri sana itakayoimarisha yale uliyojifunza na utakayoendelea kujifunza katika kujijengea falsafa mpya ya maisha yako.
Karibu upate maelezo ya semina hii nzuri;
MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu.
Hii ni semina kwa njia ya mtandao ambayo itakukumbusha kitu muhimu sana kwenye maisha yako. Kwamba wewe ni mshindi na una kila unachohitaji kushinda. Kinachokuzuia mpaka sasa ni kukosa maarifa sahihi na kuzungukwa na jamii ambayo inakulazimisha kwamba huwezi tena kushinda.
Huu ni uongo wa hali ya juu sana na umekufanya uishi maisha ambayo sio stahili kwako. Kupitia semina hii utaweka ahadi yako na nafsi yako ambayo itakuwezesha kushinda.
Nini kipya kwenye semina hii, si yale ambayo tunajifunza kila siku?
Semina hii ina mambo mengi sana mapya. Pamoja na haya unayojifunza kila siku, hapa kuna mbinu za tofauti za kuhakikisha kwamba unaishi ule ushindi uliopo ndani yako.
Kitu kikubwa sana ambacho hujawahi kupata kwenye semina nyingine ni kwamba mimi sitakufundisha, bali utakuwa unajipa ahadi wewe mwenyewe. Jinsi masomo ya semina hii yalivyoandaliwa ni kwamba utakuwa unajiambia ni kipi ambacho unafanya. Sio mimi nakwambia WEWE NI MSHINDI, bali wewe unajiambia mwenyewe MIMI NI MSHINDI. Na masomo yote kwenye semina hii yamekaa kwa muundo huo.
Kwa hiyo hii inakuwa ni ahadi ya kweli na nafsi yako, unajiambia mimi ni mshindi, hii ina nguvu zana kuliko kuambiwa wewe ni mshindi
MUUNDO WA SEMINA HII;
Semina hii itaendeshwa kwa mwezi mmoja, mwezi huu wa kumi.
Semina itaanza jumatatu ya tarehe 05/10/2015 na kumalizika ijumaa ya tarehe 30/10/2015.
Semina hii itakuwa na mafunzo 20 ambapo somo moja litatumwa kila siku kwa siku tano za wiki. Siku za mwisho wa wiki zitakuwa za kuuliza na kujibu maswali.
Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao, email, kundi la wasap na kutumiwa ujumbe mfupi.
Kwa kujiunga na semina hii;
Kila siku ya semina utatumiwa email yenye mafunzo ya semina ikiwa na hatua za kuchukua pia.
Utapata nafasi ya kuwepo kwenye kundi la wasap, ambapo utaweza kusoma masomo haya kwenye simu yako na pia kupata nafasi ya kushiriki mijadala inayoendana na hiki tunachojifunza.
Kila siku asubuhi utapata ujumbe mfupi kwenye simu yako ya mkononi ukikupa mbinu za ushindi na kukumbusha kwamba wewe ni mshindi.
Utaweza kuwasiliana nami, na hata kuuliza maswali na kujibiwa wakati wowote wa kipindi hiki cha semina.
Yafuatayo ni masomo yaliyopo kwenye semina hii;
SEMINA; MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu.
1. Nilizaliwa kushinda.
2. Maisha yangu ni jukumu langu.
3. Ninaamini ninaweza kushinda.
4. Ninapima ushindi wangu kwa malengo.
5. Mimi kama mshindi ni mwaminifu.
6. Nimejitoa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.
7. Muda ni mali ya thamani kwangu.
8. Nimezishinda hofu zote.
9. Kujifunza kila siku ndiyo nguzo yangu.
10. Nimeacha kutafuta sababu.
11. Wakatishaji tamaa hawaniyumbishi.
12. Ninafanya kile nilichopanga kufanya leo.
13. Kukosea ni sehemu ya ushindi wangu.
14. Ninakazana kuwa bora na sio kuwashinda wengine.
15. Ninajua hakuna njia ya mkato.
16. Kulaumu na kulalamika ni mwiko kwangu.
17. Mimi ni king’ang’anizi, sikubali kukata tamaa.
18. Ninashukuru kwa maisha haya ya ushindi.
19. Ninashirikiana na washindi wenzangu.
20. Ninachukua hatua mara moja.
Masomo haya 20 yameandaliwa vizuri sana kiasi kwamba kadiri unavyokwenda unaendelea kuvunja minyororo yote ambayo inakuzuia kufikia mafanikio. Kumbuka mabadiliko ya kweli kwenye maisha yako yanaanza na wewe mwenyewe, na ndio maana mafunzo haya yameandaliwa ili kukuwezesha wewe mwenyewe kubadilika, kujiahidi kwamba utashinda na baadae utashinda kweli.
CHETI CHA AHADI.
Ili kuongeza na kuweka msisitizo zaidi kwenye ahadi hii, baada ya mafunzo haya tutaandaa vyeti maalumu vya wewe kujiahidi mambo haya muhimu. Utaweka sahihi kwenye cheti hiko na kukiweka mahali ambapo kila siku unaweza kukiona na kujikumbusha kwamba wewe ni mshindi na ni mambo gani unafanya kama mshindi.
Yaani nakuhakikishia, kama utajiunga na mafunzo haya, na kuyafanyia kazi, na ukapata cheti hiki ambacho kitakuwa kinakukumbusha kila siku, hakuna kitu chochote, narudia tena, HAKUNA KITU CHOCHOTE kinachoweza kukuzuia wewe kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
GHARAMA ZA SEMINA HII.
Kwa yote haya mazuri upo tayari kulipia kiasi gani cha fedha?
Hakuna thamani unayoweza kuweka kwenye mafunzo haya, yana thamani kubwa sana ambayo huwezi kuitathmini kwa viwango vya fedha. Lakini kwa sababu wewe ni rafiki yangu, na lengo langu ni kukuona wewe unafanikiwa, utachangia mchango mdogo wa kuhakikisha semina hii inaweza kuendeshwa.
Na mchango huo utakuwa tsh elfu 30(30,000/=) kwa mafunzo ya semina. Kwa wale watakaotaka kupata vyeti vya kumbukumbu ya ahadi yao wataongeza gharama kidogo za kupata cheti kile, tutajuzana baadae.
Hii ni gharama ndogo sana ambayo huwezi kuipata kwa mafunzo kama haya ambayo utayapata.
KUJIUNGA NA MAFUNZO HAYA.
Ili uweze kushiriki mafunzo haya, unahitaji kujiunga kwa kujaza taarifa zako na kisha kulipia ada ya mafunzo.
Kujiunga na kulipia kumefunguliwa leo tarehe 18/09/2015 na mwisho wa kujiunga na kulipia itakuwa tarehe 02/10/2015. Baada ya hapo hutakuwa tena na nafasi ya kujiunga.
Ili kuhakikisha washiriki wanapata mafunzo bora, nafasi za ushiriki huwa zinakuwa chache. Hivyo ni vyema ukachukua hatua haraka.
Kujaza taarifa zako bonyeza maandishi haya na malipo fanya kwa namba zifuatazo; M PESA 0755 953 887, TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253.
Chukua hatua haraka kabla nafasi hii ya kipekee haijakupita.
Nakukaribisha sana kwenye mafunzo haya ambayo ninaamini bila ya kusita kwamba yatabadili maisha yako. Nimejitoa kuweka kila ninachojua kwenye mafunzo haya ili yawe msaada mkubwa sana kwenye maisha yako, usijaribu kabisa kuyakosa.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Unataka kuimarisha FALSAFA YAKO MPYA YA MAISHA? bonyeza maandishi haya sasa na ujiunge na mafunzo haya mazuri.